Mke wa meneja wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson amefariki dunia

Familia ya Ferguson ilithibitisha habari hiyo katika taarifa iliyotolewa kwa shirika la habari la PA Ijumaa alasiri.

Muhtasari
  • Bendera katika uwanja wa Old Trafford zimeshushwa hadi nusu mlingoti na timu za kwanza za wanaume na wanawake zitavaa vitambaa vyeusi katika michezo yao mtawalia wikendi hii.

Lady Cathy Ferguson, mke wa meneja wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84.

Familia ya Ferguson ilithibitisha habari hiyo katika taarifa iliyotolewa kwa shirika la habari la PA Ijumaa alasiri.

"Tuna masikitiko makubwa kuthibitisha kifo cha Lady Cathy Ferguson jana, aliyeacha mumewe, wanawe watatu, dada wawili, wajukuu 12 na kitukuu mmoja," ilisomeka taarifa hiyo.

"Familia inaomba faragha kwa wakati huu."

Bendera katika uwanja wa Old Trafford zimeshushwa hadi nusu mlingoti na timu za kwanza za wanaume na wanawake zitavaa vitambaa vyeusi katika michezo yao mtawalia wikendi hii.