Gavana Mwangaza aomba usaidizi katika Seneti huku kukiwa na vitisho vya kubanduliwa madarakani

Wakilishi wadi wa Meru wiki chache zilizopita walisema watawasilisha hoja ya pili ya kumshtaki

Muhtasari

• Mwangaza anamtaka Spika Amason Kingi kuuliza kwamba Kamati ya Kudumu ya Ugatuzi itasimamia mazungumzo yao ya amani

• Katika barua hiyo, Mwangaza anadai kuwa viongozi wote waliochaguliwa katika kaunti hiyo wanampinga akiwemo Naibu gavana wake Mutuma M'ithinkia

GAVANA WA MERU KAWIRA MWANGAZA
Image: KAWIRA MWANGAZA/FACEBOOK

Gavana wa Meru Kawira Mwangaza sasa anaomba usaidizi wa Seneti katika kutatua mzozo  na Wabunge wa Bunge la Kaunti na viongozi wengine, wanaoshinikiza kutimuliwa kwake kutoka madarakani.

Katika barua iliyoonekana na gazeti la The Star, Mwangaza anamtaka Spika Amason Kingi kuitaka Kamati ya Kudumu ya Ugatuzi kusimamia mazungumzo yao ya amani "Kwa ari ya maridhiano na kufahamu vyema kwamba Kamati ya Kudumu ya Seneti inayosimamia ugatuzi iko katika nafasi ya kupatanisha tofauti hizi zinazoonekana kati yakena Naibu Gavana na Bunge la Kaunti.

Mwaka jana, wakilishi wadi katika kaunti ya  Meru  walifanya hatua ya kumgatua lakini iligonga mwamba baada ya Seneti kumwokoa kutoka kwa kuondolewa madarakani mnamo Desemba 30, 2022.

Hii ilikuwa baada ya wakilishi wadi 67 kati ya 69 waliokuwa katika Bunge la Kaunti ya Meru kumtimua mnamo Desemba 14, kwa misingi mitano ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya ofisi,siku 64 tu baada ya kushika wadhifa huo.

Kamati maalum ya Seneti yenye wajumbe 11 iliyokuwa ikiongozwa na Seneta wa Kakamega Boni Khalwale ilisema hakuna madai yoyote yaliyotolewa dhidi yake ambayo yalithibitishwa na wakilishi wadi.