Sijawahi ingia chuo chochote cha uchungaji, ni Mungu aliniita - Pasta Ezekiel aiambia bunge

Ezekiel alisimulia kwamba mungu ndio upeana kipawa cha uchungaji

Muhtasari

•Mchungaji huyo alindamana na mawakili wake wakiongozwa na Danstan Omari, Cliff Ombeta, Samson Nyaberi, na Shadrack Wambui

Pasta Ezekiel
Pasta Ezekiel
Image: Screengrab//CitizenTv

Mhubiri na kiongozi wa kanisa la  New Life Prayer Center Ezekiel Odero  alifika mbele ya kamati maalum ya seneti inayochunguza uhusiano wake na mhubiri mwenye utata Paul Mackenzie.

Mchungaji huyu aliandamana na mwenzake Pasta  Pius Muiru ambaye alimtaja kuwa Baba wake wa kiroho.

Ezekiel Odero alisimulia kwenye kamati hii kuwa yeye kwa maisha yake yote katika umri wake ajawahi kujiunga na chuo chochote cha mafunzo ya uchangaji mbali na kuwa kiongozi wa kanisa mwenye wafuasi wengi.

"Mungu ndio alinibariki na kipawa cha uchungaji mimi uomba mungu na chochote nataka unibariki nacho kusimamisha kanisa kubwa kama New life Prayer Center ni neema ya wito wa mwenyenzi mungu",alisema.

Mchugaji huyu alikubwa na tetesi baada ya uvumi kutokea kwamba kituo cha runinga anachopeperusha matangazo ilikuwa ameimiliki kutoka kwa mchugaji Mackenzie.

Odero na Muiru wataandamana na mawakili wao wakiongozwa na Danstan Omari, Cliff Ombeta, Samson Nyaberi, na Shadrack Wambui.

Kamati hiyo ya seneti inachunguza hali iliyopelekea vifo vya wafuasi wa mhubiri mwenye utata wa Kanisa la Good News International, Paul Mackenzie, ambaye kwa sasa anazuiliwa na polisi kwa makosa kashaa ikiweno mauaji na unyanyasaji wa watoto.