Sijawahi kutumia pesa za kanisa kwa manufaa binafsi-Pasta Ezekiel asema

Ezekiel alikiri kwamba makanisa mengi yana wakati mgumu wa kufafanua mambo yanayohusiana na matoleo ya kanisa.

Muhtasari

•Akiwa amefika mbele ya Kamati a ya Seneti inayochunguza vifo vya Shakahola mnamo Oktoba 13, kasisi huyo alifichua kwamba hatawahi kugusa matoleo ya kanisa.

•"Sijawahi  kutumia pesa za zaka ya  kanisa kwa manufaa binafsi. Nimemjulisha mke wangu na watoto wangu hakuna mtu atakayefaidika na pesa za kanisa. Nina biashara ya kuku ambayo uniwezesha kusomesha watoto wangu ,hivyo hakuna haja kutumia pesa za kanisa,"

Pata Ezekiel Odero,New Life Prayer Center
Pata Ezekiel Odero,New Life Prayer Center
Image: The star

Mwazilishi wa kanisa la New Life Prayer  Center Ezekiel Odero,amekana madai ya kutumia pesa za zaka na kusema kwamba  hategemei Sadaka, kwani yeye  hutengeneza Pesa kwa Biashara ya kuku anaofuga.

Mchungaji Odero amesema  kuwa hajawahi kutumia pesa za kanisa kujinufaisha binafsi.

Akiwa amefika mbele ya Kamati a ya Seneti inayochunguza vifo vya Shakahola mnamo Oktoba 13, kasisi huyo alifichua kwamba hatawahi kugusa matoleo ya kanisa.

Ezekiel alifichua kwamba alikuwa amefahamisha familia yake kwamba hakuna hata mmoja ambaye angeruhusiwa kutumia toleo la kanisa. Mhubiri  alisema kwamba alikuwa ameanzisha biashara ya kuku, na mapato yake yangetumika kusomesha watoto wake watatu.

"Sijawahi  kutumia pesa za zaka ya  kanisa kwa manufaa binafsi. Nimemjulisha mke wangu na watoto wangu hakuna mtu atakayefaidika na pesa za kanisa. Nina biashara ya kuku ambayo uniwezesha kusomesha watoto wangu ,hivyo hakuna haja kutumia pesa za kanisa," Ezekiel alisema.

Ezekiel alikiri kwamba makanisa mengi yana wakati mgumu wa  kufafanua mambo yanayohusiana na matoleo ya kanisa.

Mhubiri huyo alitoa changamoto kwa kamati kuwaita wahubiri wengine kote nchini na kuwawekea jukumu juu ya kile ambacho wamefanya na toleo wanalopokea.

"Unajua kuwa wakati mwingine wachungaji wanaogopa kusema ukweli juu ya sadaka, lakini nilikuja hapa kukuambia ukweli juu ya sadaka, Ikiwa sio nyingi, unafanya nini nayo? Na pia naomba uulize ni watu wangapi kanisani kwako na unafanya nini na sadaka,” Ezekieli aliuliza.

Hapo awali, Ezekiel aliwataka polisi kumlinda yeye na waumini wake atakapoheshimu wito wa kufika mbele ya Seneti kuhojiwa.

Kupitia kwa wakili wake, Danstan Omari, Ezekiel alimwandikia Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kati, akiomba maafisa wa kutosha wa polisi kwa ajili ya umati ulioandamana naye huku wabunge wakimhoji.