Uchunguzi wa Shakahola: Mhubiri Ezekiel afika mbele ya Kamati ya Seneti

Kamati hiyo inachunguza hali iliyopelekea vifo vya wafuasi wa mhubiri mwenye utata wa Kanisa la Good News International, Paul Mackenzie.

Muhtasari

• Kamati hiyo inachunguza hali iliyopelekea vifo vya wafuasi wa mhubiri mwenye utata wa Kanisa la Good News International, Paul Mackenzie

Mchungaji Ezekiel Odero.
Mchungaji Ezekiel Odero.
Image: MAKTABA

Mhubiri na kiongozi wa kanisa la The New Life Prayer Center Ezekiel Odero na mhubiri mwenzake Pius Muiru leo wanafika ya Kamati maalum ya Seneti. 

Kamati hiyo inachunguza hali iliyopelekea vifo vya wafuasi wa mhubiri mwenye utata wa Kanisa la Good News International, Paul Mackenzie, ambaye kwa sasa anazuiliwa na polisi kwa makosa kashaa ikiweno mauaji na unyanyasaji wa watoto. 

Odero na Muiru wataandamana na mawakili wao wakiongozwa na Danstan Omari, Cliff Ombeta, Samson Nyaberi, na Shadrack Wambui.