Wakili ghushi Brian Mwenda aliyemwakilisha aliyekuwa kiongozi wa Mungiki akamatwa

Brian alikamatwa na Chama cha Wanasheria cha Kenya Tawi la Nairobi ,Rapid Action Team (RAT) kwa uwongo

Muhtasari

• Video za Brian Mwenda akimwakilisha kiongozi wa zamani wa Mungiki katika kesi iliyoonyeshwa kwenye televisheni zimeibuka mtandaoni

• Alikamatwa na Chama cha Wanasheria cha Kenya Tawi la Nairobi cha kuchungulikia maswala ya dhalula kwa uhongo

Brian Mwenda
Image: picha Hisani

Siku ya Alhamisi, mamlaka ya Kenya ilimzuilia Brian Mwenda, wakili mlaghai ambaye alijitambulisha kwa uwongo kama Wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya.

Ripoti zinaonyesha kuwa kabla ya kukamatwa Mwenda alishinda kesi 26 mbele ya Majaji wa Mahakama Kuu, Mahakimu na Majaji wa Mahakama ya Rufaa na alishinda zote.

Alikamatwa na Chama cha Wanasheria cha Kenya Tawi la Nairobi Rapid Action Team (RAT) kwa kujifanya wakili.

Mwigaji huyu alikamatwa timu ya kupambana ya maswala ya dhalura ilipopokea malalamiko ya umma kuhusu vitendo vyake vya ulaghai.

Kulingana na rekodi za LSK, yeye si wakili na hana leseni ya kutekeleza sheria nchini Kenya. Katika taarifa ilisema kwamba Brian hakuwa wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya wala si mwanachama wa LSK Tawi la Nairobi.

Imefahamishwa kwa LSK Tawi la Nairobi kupitia Timu ya Rapid Action (RAT), kwamba mtu aliye kwenye picha amekuwa akijiwasilisha na kujiendesha kama Wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya na mwanachama wa LSK Tawi la Nairobi

Anazuiliwa katika makao makuu ya timu ya kuchuguza mawakili  akisubiri uchunguzi zaidi, Wakati uo huo, video za Brian akimwakilisha kiongozi wa zamani wa Mungiki katika kesi iliyoonyeshwa kwenye televisheni zimeibuka mtandaoni.