Mwanamke mwenye gadhabu amkabili askari wa kaunti, Nairobi

Video hiyo inaonyesha mwanamke huyo akijibizana na afisa huyo wa kanjo kufuatia mzozo wa kuegeza gari.

Muhtasari

• Tukio hilo limezua mijadala mitandaoni kuhusu jinsi raia wa wanavyotendewa na maafisa wa kanjo katika pilkapilka za kukusanya ushuru.

• Katika video hiyo, TikToker aliyetambulika kama Ntazola Gloria anaweza kuonekana akipinga jaribio la afisa huyo kumkamata kwa kuingia ndani ya gari lake.

Afisa wa kanjo Nairobi Hisani TikTok
Afisa wa kanjo Nairobi Hisani TikTok

Video inayoonyesha mzozo mkali kati ya TikToker wa Kenya na afisa wa kanjo kuhusu suala la maegesho katika Wilaya ya Kati ya Biashara ya Nairobi imezua hisia mbalimbali kutoka kwa Wakenya.

Video hiyo inaonyesha mwanamke huyo akijibizana na afisa huyo wa kanjo kufuatia mzozo wa kuegeza gari.

Tukio hilo limezua mijadala mitandaoni kuhusu jinsi raia wa wanavyotendewa na maafisa wa kanjo katika pilkapilka za kukusanya ushuru.

Katika video hiyo, TikToker aliyetambulika kama Ntazola Gloria anaweza kuonekana akipinga jaribio la afisa huyo kumkamata kwa kuingia ndani ya gari lake.

Ntazola aliwastumu maafisa wa kanjo akitaka kujua mbona hasa wanaifanya tabia hiyo ya kuwanyanyasa watu kukolea,akilazimika kuweka msimamo mkali huku akimwambia afisa huyo kuwa angeandamana na yeye popote alipokuwa anaenda.

“Mbona mko na hiyo tabia? Hicho ni kitu cha kukaa kwenye gari langu; tunaenda pamoja popote ninapoenda,” alisema kwa ujasiri kwenye video hiyo.

Video hiyo inaonyeshwa na TikToker mwanzoni ikijaribu kumshawishi afisa wa kanjo asimtie kizuizini au kukamata gari lake, lakini juhudi zake zilikabiliwa na kukataa kabisa kutoka kwa afisa huyo.

“Nakupeleka kwangu sasa hivi, na nitakupeleka na gari hili, kwa nini uliingia kwenye gari langu?"

Malumbano hayo yanaendelea huku pande hizo mbili zikizozana kuhusu masuala yanayohusu kanuni za maegesho ya magari.

“Tunaenda nawe kule niendako, mbwa wewe. Unasumbua Wakenya,hauoni watu wako na mawazo. Kwa nini uliingia kwenye gari langu? Ninakuambia, wewe ni mbwa, siendi hata kazini, tunaenda nawe. Kwa nini uliingia kwenye gari langu? Wewe ni afisa wa polisi wa trafiki?" Alishangaa.

Kujibu, afisa wa kanjo anajaribu kumsihi mwanamke  huyo amruhusu kuondoka lakini zuhudi zake hazikuvua dafu.

“Ninakupeleka mpaka Ng’ong. Una tabia mbaya sana. Siwezi kuegesha gari langu? uMbona uliingia, si nilikuambia nataka kuegesha gari langu? Kwa nini ulikataa? 

Haya yanijiri wakati ambapo maafisa wa kanjo waliwavamia wachuuzi wanaofanya biashara ndogondogo jijini Nairobi,ambao wamekashifiwa na baadhi ya viongozi wa taifa pamoja na wakenya wenye ghadhabu.

Video hii imepata usikivu mkubwa na udadisi kutoka kwa Wakenya ambao wana hamu ya kujifunza zaidi kuhusu matokeo ya "safari hii ya barabarani" isiyo ya kawaida.