Rais William Ruto atia saini miswada ya Bima mpya ya Afya UHC

Serikali inasema itafanya huduma za afya kuwa nafuu zaidi na kupatikana kwa Wakenya maskini.

Muhtasari
  • Wengine pia wanahofia kuwa mfuko mpya wa huduma ya afya utakumbwa na ufisadi, kama ule uliopo, ikimaanisha kwamba mara nyingi hawawezi kupata huduma za afya wanazostahili.
RAIS WILLIAM RUTO

Rais William Ruto ameidhinisha sheria tata ambayo italeta mabadiliko makubwa zaidi ya sekta ya afya katika zaidi ya miaka 20.

Mpango wake unahusu kukuza huduma ya afya kwa wote, na unahitaji wafanyakazi wote kuchangia 2.75% ya mishahara yao kwa mfuko mpya wa afya.

Serikali inasema itafanya huduma za afya kuwa nafuu zaidi na kupatikana kwa Wakenya maskini.

Lakini imeonekana kutopendwa na Wakenya wengi, wanaoiona kama ushuru mpya.

Wanasema ni hatua ya hivi punde zaidi katika msururu wa hatua ambazo Bw Ruto ameanzisha na hivyo kuzidisha mzozo wa gharama ya maisha, licha ya kwamba alishinda uchaguzi mwaka jana kwa ahadi ya kupunguza matatizo ya kifedha ya familia.

Wengine pia wanahofia kuwa mfuko mpya wa huduma ya afya utakumbwa na ufisadi, kama ule uliopo, ikimaanisha kwamba mara nyingi hawawezi kupata huduma za afya wanazostahili.

Lakini bunge limemuunga mkono Bw Ruto, kupitisha Mswada wa Bima ya Afya ya Jamii, pamoja na miswada mingine mitatu ya afya, mnamo Jumanne.

Kwa sasa, Wakenya hulipa kati ya shilingi 150 za Kenya ($1; £0.80) na shilingi 1,700 kila mwezi kwa Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya (NHIF).

Itabadilishwa na mfuko mpya, na kiwango cha chini cha mchango kimewekwa kuwa maradufu na wafanyikazi wengi wanaolipwa mishahara wakichangia sehemu kubwa zaidi ya malipo yao.