Mungu ni mwaminifu kwangu ameniondolea changamoto tele pasta Ezekiel Odero asema

Nyota ya mchungaji Ezekiel yang'aa baada hatima ya kesi kukamlika

Muhtasari

•Ezekiel Odero alishtakiwa kortini kwa shutma  za kuwa na urafiki na mchungaji mwenye utata Paul Mackenzie aliyedaiwa kuhusika na vifo vya watu zaidi ya 45O kesi ambayo ilikosa ushaidi na kutupliwa mbali na mahakama

katika kanisa la Mchungaji Ezekiel Odero huko Mavueni, kaunti ya Kilifi, Jumatatu, Oktoba 16, 2023.
Kamati maalum ya Seneti kuhusu mauaji ya Shakahola katika kanisa la Mchungaji Ezekiel Odero huko Mavueni, kaunti ya Kilifi, Jumatatu, Oktoba 16, 2023.
Image: JOHN CHESOLI

Saa chache baada ya mahakama kutupilia mbali kesi dhidi ya mhubiri Ezekiel Odero alimshukuru Muumba wake kwa kuwa mwaminifu ndani ya maisha yake baada ya kutopatikana na  kosa kwa kesi iliyomkumba.

Kiongozi huyu wa Kanisa alitoa kauli hii baada ya kuandaa ibada ya kuwaombea wafuasi wake wanaofuatilia mahubiri yake  kwenye Runinga na  mitandao ya kijamii.

"Mungu ni mwaminifu kwa mja wake ,hakika ameniondolea huofu wote na kusafisha Jina langu kupitia kanisa lake,nilipitia Mengi, kanisa likafugwa kwa siku chache,mahubiri yangu kwenye Runinga yakakatizwa kwa muda,"alisema.

Mchungaji huyu alisimulia jinsi kongamano za moambi alizoweka kwa kaunti tofauti zilikatizwa licha ya kuwa alikuwa amezigharamikia.

"Wakati ufika kwa maisha ya mwanadamu jina litapakwa tope ila   Mungu ni mwaokozi wa wote wanaomtumaina mapito haya yalikuwa sehumu Mungu kuonesha upendo wake kwa kanisa lake,"alisema Ezekiel.

Kiongozi huyu wa kanisa la New Life Prayer Center Mavueni  alionesha ushaidi wa cheti cha korti alichopewa kwa wafuasi wake akishukuru maafasi wa kitengo cha kupambana na ufisadi kwa kukamilisha uchunguzi wao kwa haraka na Korti kumuachiliia  Huru.

Ezekiel Odero alishtakiwa kortini kwa shutma  za kuwa na urafiki na mchungaji mwenye utata Paul Mackenzie aliyedaiwa kuhusika na vifo vya watu zaidi ya 45O kesi ambayo ilikosa ushaidi na kutupliwa mbali na mahakama.

Mchungaji huyu pia alikesiwa kuwa na makavani ndani ya kanisa lake jambo ambalo lilichuguzwa na kamati ya seneti na kubaini kuwa kilikuwa chumba cha kusambaza umeme.