Ni pigo kwa wasafiri wanaojiandaa kwa shamrashamra za musimu wa krismasi mwaka huu baada shirika la reli la kisasa SGR kutangaza kutoza nauli za juu kwa yeyote anayetaka kupata huduma za usafiri kupitia shirika hili.
Wakenya wengi hupendelea huduma za shirika hili la reli ya kisasa kwa jinsi ambavyo ilitoza nauli za chini kwa usafiri ila kwa sasa nauli katika maeneo yote inayopeana huduma zake za usafiri imepadisha kwa asilimia 50.
Katika hakiki ya hivi punde, abiria wa Mombasa sasa watalipa Sh1,500 kuanzia Januari 1, 2024, kutoka Sh1,000 nauli hii ikiwa imepanda kwa shilingi mia tano.
Kwa wasafiri wale wanaotaka kusafiri na daraja la kwanza, watalazimika kulipa Sh4,500, kutoka Sh3,000 nauli hii ikipadishwa kwa shiliingi elfu moja mia tano.
Hata hivyo shirika hili limebainisha kuwa tikiti zilizonunuliwa kabla ya wakati huo, hata hivyo, hazitaathirika.
Nauli ya wasafiri kutoka Kibwezi hadi Mombasa itagharimu Sh890 huku Voi hadi Mombasa ikigharimu Sh440.
Bei hizo ziliorodheshwa upya kwa Huduma ya abiria ya Madaraka Express, Huduma ya Reli ya Nairobi Commuter, Treni ya Safari ya Kisumu na Treni ya Safari ya Nanyuki.