Wacheni kuchezea maisha ya Wakenya - Sonko awaambia magavana

"Wacheni mchezo wa kulia kama watoto wadogo jitokezeni msaaidie wananchi wanaumia si kila mara mnafaa kutengemea serekali kuu," alisema.

Muhtasari

• Hata hivo Sonko aliwataka madereva kuwa waangalifu wakati huu wa mafuriko akisema kuwa baadhi ya madereva wanahatarisha maisha ya abiria.

Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko
Image: Facebook//Mike Sonko

Aliyekuwa gavana wa kaunti ya Nairobi, Mike Mbuvi Sonko  amewataka magavana kujisatiti kwa kuwasaidia wananchi wakati huu Wakenya wengi wameadhirika na mafuriko ya mvua ambayo inaendelea kunyesha nchini

Sonko kupitia mahojiano ya moja kwa moja na wanahabari aliwashauri magavana kuwacha kasumba ya kutengemea serekali kuu kwa kila jambo akisema kuwa ni jukumu la kila kaunti kuwa limetenga pesa za dharura wakati wa majanga.

"Wacheni mchezo wa kulia kama watoto wadogo jitokezeni msaaidie wananchi wanaumia  si kila mara mnafaa kutengemea serekali kuu zile pesa ambazo kaunti uekeza ili kupambana na majanga ndio wakati mzuri zinaa kutumuka,"alisema.

Gavana huyo wa zamani alisema hayo wakati alipokuwa ameandamana na viongozi wengine kusaindia familia ambazo zilipoteza wapedwa wao baada ya kuzobwa na maji wikendi hii.

Hata hivo Sonko aliwataka madereva kuwa waangalifu wakati huu wa mafuriko akisema kuwa baadhi ya madereva wanahatarisha maisha ya abiria kwa kuwavukishwa kwa mito ambayo imeadhirika na mafuriko.

"Kuna madereva wanajifanya hodari kuvukisha magari kwa sehumu ambazo nyingi za daraja zimebebwa na maji madereva kama hao wanafaa kukomeshwa kwani maisha ya wanadamu ni ya maana sana",alisema.