Mkurugenzi wa Epra Daniel Kiptoo aponea jela, Mahakama yasema hana hatia kipuza agizo la korti

Katika uamuzi uliofanywa Novemba 28, Jaji wa Mahakama Kuu Christine Meoli alisema hakuna ushahidi wa kutosha wa kudhibitisha mashataka hayo.

Muhtasari

• Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli ilikuwa imeshutumiwa kwa kutotii maagizo ya mahakama kuhusu kupandisha bei ya mafuta mwezi Julai.

• "Tunampata Daniel Kiptoo hana hatia ya dharau. Tunashikilia kuwa mshirika huyo hakuwa na ufahamu wa agizo hilo wakati alipotoa taarifa kwa vyombo vya habari," 

Daniel Kiptoo Mkurugenzi EPRA
Daniel Kiptoo Mkurugenzi EPRA
Image: HISANI

Mkurugenzi Mkuu wa EPRA Daniel Kiptoo ameondolewa lawama ya kupuuza agizo la mahakama.

Mamlaka ya Udhibiti wa kwai na Petroli (EPRA) ilikuwa imeshutumiwa kwa kutotii maagizo ya mahakama na kutekeleza kudi mpya ya ushuru wa ubora wa bidhaa (VAT) kwenye mafuta mwezi Julai.

Katika uamuzi uliofanywa Novemba 28, Jaji wa Mahakama Kuu Christine Meoli alisema hakuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kosa la kupuuza agizo la korti. 

"Tunampata Daniel Kiptoo bila hatia ya dharau. Tunashikilia kuwa hakuwa na ufahamu wa agizo hilo wakati alipotoa taarifa kwa vyombo vya habari," aliamua.

"Zaidi ya hayo, waombaji hawajatoa ushahidi wowote unaoonyesha kutotii amri kwa makusudi."aliongeza.

Kesi hiyo ilitokana na amri ya mahakama iliyotolewa Juni 30, 2023, na Jaji Mugure Thande katika kesi dhidi ya  mswada  wa Sheria ya Fedha, 2023.

Licha ya maagizo hayo kuzuia kutekelezwa kwa Mswada huo na kutozwa ushuru wa asilimia 16 kwa bidhaa za mafuta, Kiptoo alichapisha taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mabadiliko ya bei ya mafuta.

Kufuatia hayo, Seneta wa Busia Okiya Omtatah aliwasilisha ombi la kuishutumu Epra kwa kukosa kufuata maagizo ya mahakama.

Omtatah aliwaambia Majaji David Majanja, Christine Meoli na Lawrence Mugambi kwamba Epra ilikuwa na dharau.

Alisema, kwa vile tayari ilikuwa imeshapanga kuweka bei mpya ya mafuta, kabla ya Mahakama ya Rufaa kuondoa amri zinazozuia kutekelezwa kwa Sheria hiyo Julai 28.

Omtatah alisema aliwasilisha maagizo ya mahakama kwa Kiptoo kupitia barua pepe na kupitia WhatsApp, akimsihi asitekeleze mabadiliko hayo ambayo yalisababisha ongezeko la bei za mafuta kutoka asilimia 8 hadi 16.

Seneta huyo aliitaka mahakama kumfunga Kiptoo kwa miezi sita kwa kukiuka maagizo.

Wakili wa Kiptoo hata hivyo aliambia mahakama kuwa si EPRA wala bosi wake wanaofahamu kuhusu maagizo hayo kwa vile bado yalipaswa kuzuiliwa katika kesi ya Sheria ya Fedha.

Alisema Kiptoo alikuwa akitekeleza majukumu yake tu siku alipotangaza ongezeko la bei za mafuta, na anaandamwa kwa ufanisi wake.

Baada ya uhakiki, mahakama iligundua kuwa kulikuwa na mazungumzo ya WhatsApp kati ya Omtatah na Kiptoo, ambayo hayakupingwa.

Kiptoo hata hivyo aliambia mahakama kuwa wakati akipokea agizo hilo, alikuwa tayari ametoa taarifa kwa vyombo vya habari akitekeleza majukumu yake kama  Mkurugenzi.