logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mlinzi wa nyumbani wa Kalonzo afariki akidaiwa kunywa sumu

Haijabainika ni kwa muda gani afisa huyo alikuwa akifanya kazi nyumbani kwa Kalonzo.

image
na Davis Ojiambo

Habari28 November 2023 - 08:31

Muhtasari


  • •Jumapili wenzake walimsikia akilia kwa maumivu ndani ya nyumba yake katika boma la Kalonzo na kuharakisha kujua kilichokuwa kikiendelea
Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, ambaye alipoteza mlinzi katika nyumba yake kijijini Tseikuru huko Kitui Picha: MUSEMBI NZENGU

Polisi mjini Kitui wanachunguza kifo cha afisa wa polisi aliyepewa jukumu la kulinda nyumba ya  kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka.

Siku ya Jumatatu, kamanda wa polisi kaunti ya Kitui Leah Kithei alisema polisi huyo alisemekana kujitoa uhai kwa kunywa sumu.

Akizungumza katika afisi yake mjini Kitui, Kithei alisema kuwa mwendo wa saa nane unusu siku ya Jumapili wenzake walimsikia akiwa katika maumivu ndani ya nyumba yake katika boma la Kalonzo na kuharakisha kujua kilichokuwa kikiendelea.

"Walimpata amelala bila fahamu kwenye kitanda chake na kumkimbiza katika Hospitali ya Mumoni Nursing iliyo karibu na kituo cha biashara cha Tseikuru ambako alifariki alipokuwa akipewa matibabu," Kithei alisema.

Alisema kuwa  hakuweza kutaja utambulisho wa afisa huyo ambaye kwa sababu hakuwa na uhakika kama jamaa zake wa karibu walikuwa wamefahamishwa kuhusu kifo chake.

"Ninachoweza kusema ni kwamba tumeanza uchunguzi kuhusu kifo hicho, Wacha tusubiri hadi mwisho wa uchunguzi ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa maiti ili ukweli ujulikane," Kithei alisema.

Haijabainika ni kwa muda gani afisa huyo alikuwa akifanya kazi katika nyumba ya mashambani ya Kalonzo kwani gazeti la The Star ,halikuweza kumfikia kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Tseikuru Fredrick Onyango ili atoe maoni yake. Onyango alisemekana kuwa hayuko likizoni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved