Wakenya Kuendelea Kulipa Ushuru wa Nyumba hadi Januari – Mahakama kuu yaamuru

Haya yanajiri baada ya mahakama kutangaza tozo hiyo kuwa kinyume na katiba, ikisema inakiuka Ibara ya 10, 2 (a) ya Katiba.

Muhtasari

• Amri za kusitisha kesi hiyo zinafuatia ombi la Walalamikiwa katika kesi hiyo wakiongozwa na wakili George Murugara kwa muda wa siku 45 ili kutekeleza uamuzi wa mahakama.

• “Tunagundua kuwa kuanzishwa kwa marekebisho ya tozo ya nyumba katika kifungu cha 84 kunakosa mfumo wa kisheria unaokiuka ibara ya 10 ya katiba,

Jaji Davida Majanja
Jaji Davida Majanja
Image: HISANI

Wakenya wataendelea  kutozwa ushuru wa Nyumba  baada ya Mahakama kutoa amri ya kwa serikali kuendelea kutekeleza sheria hiyo hadi Januari 10, 2024.

Haya yanajiri baada ya mahakama kutangaza tozo hiyo kuwa kinyume cha sheria, ikisema inakiuka Ibara ya 10, 2 (a) ya Katiba.

Amri za kusitisha kesi hiyo zinafuatia ombi la Walalamikiwa katika kesi hiyo wakiongozwa na wakili George Murugara kwa muda wa siku 45 ili kutekeleza uamuzi wa mahakama.

"Katika siku hizo 45, ninakuomba usitishe ukandamizaji wa matokeo hayo mahususi katika hukumu na amri yoyote ili kusubiri kuwasilishwa kwa maombi rasmi chini ya Kanuni za Mutunga na Kanuni za Mahakama ya Rufaa,”alisema Murugara.

"Sababu ni kwamba, kwanza, tunapaswa kufanya marekebisho yanayohitajika kwa utaratibu wa serikali wa kutoza ushuru ndiposa kusiwe na chama au shirika la serikali litakaloshotakiwa kwa dharau ,”aliongeza

Jopo la majaji watatu lililojumuisha Majaji David Majanja, Lawrence Mugambi na Christine Meoli pia lilitangaza vifungu vya 84, 72 hadi 78 vya Sheria ya Fedha kuwa batili.

“Tunagundua kuwa kuanzishwa kwa marekebisho ya tozo ya nyumba katika kifungu cha 84 kunakosa mfumo wa kisheria unaokiuka ibara ya 10 ya katiba, kwamba tozo kwa watu walio katika ajira rasmi bila ya uhalali ni ubaguzi na hauna mantiki,” Jaji Majanja alisoma hukumu hiyo.

Ushuru huo ambao ni nguzo kuu katika Sheria ya Fedha, ulianza kukatwa kutoka kwa Wakenya walioajiriwa mnamo Julai, huku Mamlaka ya Ushuru ya Kenya (KRA) ikiidhinishwa kuwa wakala wa kukusanya.

Waajiri wamekuwa wakituma mchango wao wa asilimia 1.5 pamoja na kiwango sawa kwa wafanyakazi wao pia.

Serikali ilikuwa imetaja kwamba makato hayo ambayo hayakutarajiwa yangewawezesha kufikia mpango wao madhubuti wa kujenga nyumba za bei nafuu kwa Wakenya wa kipato cha chini.