logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maadhimisho ya Jamhuri, Wakenya kuingia mbuga za wanyama na makavazi ya kitaifa bila malipo siku ya Jamhuri

Kiingilio hicho bila malipo kitatumika kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni.

image
na Radio Jambo

Habari08 December 2023 - 14:22

Muhtasari


• Fursa hiyo ni kwa raia wa Kenya walio na uthibitisho wa utambulisho na watoto wanaoandamana na wazazi au walezi au wanafamilia ambao wana uthibitisho wa utambulisho.

Serikali imetangaza kuwa Wakenya wataruhusiwa kuingia mbuga zote za kitaifa, na makavazi bila malipo mnamo Desemba 12 huku Kenya ikiadhimisha miaka 60 ya uhuru. 

Tangazo hilo lilitolewa na waziri wa Utalii na Wanyamapori, Dkt Alfred Mutua siku ya Ijumaa.

Serikali imetowa wito kwa wananchi kutumia fursa hiyo kujivinjari na kutembelea maeneo mbali mbali ya turathi za kitaifa ili kung’amua urembo wa nchi yao.  

"Fursa hii pia itakupa nafasi kuzuru mbuga za baharini, matembezi ya safari, na vituo vya kuwatunza watoto yatima wa wanyama. Ofa hiyo ni kwa raia wa Kenya walio na uthibitisho wa utambulisho na watoto wanaoandamana na wazazi au walezi au wanafamilia ambao wana uthibitisho wa utambulisho," alieleza.

Kiingilio hicho bila malipo kitatumika kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni, kipindi ambacho Mutua anasema kitatoa muda wa kutosha kwa wananchi kujionea urembo asili wa Kenya.

Hata hivyo, Dkt Mutua alisisitiza umuhimu wa kufuata sheria wakati wa ziara hiyo.

Hifadhi za kitaifa ni pamoja na Hifadhi ya Kitaifa ya Aberdare, Amboseli, Arabuko Sokoke, Central Island, Chyulu Hills, Hell's Gate, Hifadhi ya Kitaifa ya Bahari ya Kisite-Mpunguti, Hifadhi ya Kitaifa ya Kora, Hifadhi ya Kitaifa ya Ziwa Nakuru, Hifadhi ya Kitaifa ya Bahari ya Malindi. Hifadhi na Hifadhi ya Kitaifa ya Malka Mari. 

Nyingine ni Hifadhi ya Taifa ya Masai Mara, Meru, Mbuga ya Bahari ya Mombasa, Mbuga ya Kitaifa ya Mlima Elgon, Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kenya, Hifadhi ya Taifa ya Mlima Longonot, Hifadhi ya Taifa ya Nairobi, Hifadhi ya Taifa ya Ol Donyo Sabuk, Hifadhi ya Kitaifa ya Ruma, Hifadhi ya Saiwa Swamp, Sibiloi. Tsavo Mashariki na Magharibi na Hifadhi ya Kitaifa ya Watamu Marine.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved