Je! umeona vipepeo weupe? Wamevamia mashamba ya maua Naivasha

Wataalamu wa wadudu wanachunguza hali ili kubaini ikiwa zina hatari hasa kwa maua yanapobadilikabadilika.

Muhtasari

• Vipepeo wamevamia nyumba za kukuza maua huko Naivasha/Nakuru, siku chache tu kabla ya Siku ya Wapendanao.  

Umeona vipepeo hawa weupe? Wamevamia nyumba za kukuza maua huko Naivasha/Nakuru, siku chache tu kabla ya Siku ya Wapendanao.  

Wataalamu wa wadudu wanachunguza hali ili kubaini ikiwa zina hatari hasa kwa maua yanapobadilikabadilika. 

Mkurugenzi Mtendaji wa muungano wa mazao freshi Okisegere Ojepati anasema wakulima wametakiwa kuacha aina yoyote ya kunyunyizia dawa huku wanasayansi wakiwasili.  "Vipepeo hutaga mayai wanapopita.

Mayai yatageuka viwavi muda si mrefu. Hebu tuchunguze mimea yetu kwa uangalifu na kunyunyizia inapobidi," Wachira Kaguongo - Mkurugenzi Mtendaji, Baraza la Kitaifa la Viazi Kenya anasema.