China: Meli yagonga daraja na kutumbukiza magari kwenye mto Guangzhou

Ajali hiyo iliua watu wawili na kujeruhi mmoja. Watatu bado hawajapatikana, vyombo vya habari vya serikali vilisema.

Muhtasari

• Nahodha wa meli hiyo amekamatwa na watu wanaoishi katika eneo hilo wamehamishwa.

• Picha kwenye kituo cha utangazaji cha CCTV zinaonyesha sehemu ya daraja ikiwa imevunjika, huku meli ikiwa imenasa chini yake. Meli hiyo haikuonekana kubeba mizigo.

• Mnamo Oktoba 2021, mamlaka ya mkoa ilikuwa imetambua hitaji la kujenga "vifaa vya kuepusha mgongano" ili kuhakikisha usalama wa muundo wa daraja.

Meli ya mizigo iligonga daraja nchini China, na kutumbukiza magari mtoni.
Meli ya mizigo iligonga daraja nchini China, na kutumbukiza magari mtoni.

Meli ya mizigo iligonga daraja katika mji wa kusini wa China wa Guangzhou mapema Alhamisi, na kutumbukiza magari matano likiwemo basi la umma ndani ya mto huo.

Ajali hiyo iliua watu wawili na kujeruhi mmoja. Watatu bado hawajapatikana, vyombo vya habari vya serikali vilisema.

Picha kwenye kituo cha utangazaji cha CCTV zinaonyesha sehemu ya daraja ikiwa imevunjika, huku meli ikiwa imenasa chini yake. Meli hiyo haikuonekana kubeba mizigo.

Tukio hilo lilitokea saa 05:30 kwa saa za ndani (21:30 GMT).

Nahodha wa meli hiyo amekamatwa na watu wanaoishi katika eneo hilo wamehamishwa, kulingana na Beijing News, ikinukuu mamlaka ya wilaya.

Daraja hilo lilipaswa kuboreshwa lakini mipango imeahirishwa mara tatu, CCTV iliripoti.

Mnamo Oktoba 2021, mamlaka ya mkoa ilikuwa imetambua hitaji la kujenga "vifaa vya kuepusha mgongano" ili kuhakikisha usalama wa muundo wa daraja.

Awali utaratibu huo ulipangwa kukamilika Septemba 2022, lakini tarehe ya mwisho iliongezwa hadi Agosti 2023, na baadaye hadi Agosti mwaka huu.