Mwili wa mwanamke wapatikana umetupwa City Park, Nairobi

Mikono yake ilikuwa imefungwa kwa kamba mgongoni na alikuwa na majeraha usoni.

Muhtasari

•Polisi wanasema mwanamke huyo ambaye ametambuliwa kama Rosemary Shikoku, 35 alipatikana amekufa Jumapili katika bustani hiyo.

•Sababu ya mauaji hayo bado haijajulikana na hakuna mtu aliyekamatwa hadi sasa, polisi walisema.

crime scene
crime scene

Mwanamke mmoja amepatikana ameuawa na mwili wake kutupwa katika bustani ya City Park, katika mtaa wa Parklands jijini Nairobi.

Polisi wanasema mwanamke huyo ambaye ametambuliwa kama Rosemary Shikoku, 35 alipatikana amekufa Jumapili katika bustani hiyo.

Mikono yake ilikuwa imefungwa kwa kamba mgongoni na alikuwa na majeraha usoni.

Mwanamume mmoja ambaye alikuwa ameingia kwenye bustani hiyo aliona mwili huo na kuwaarifu polisi.

Polisi walisema begi linaloshukiwa kuwa mzigo wake ikiwa na kitambulisho cha kusubiri na karatasi ya polisi iliyotolewa katika kituo cha polisi cha Kamukunji ilipatikana kando ya mwili huo.

Pia kwenye begi hilo kulikuwa na nguo za aina mbalimbali kando ya mwili wake.

Polisi walisema mauaji hayo yanaonekana kutekelezwa sehemu nyingine na mwili ulisafirishwa hadi eneo la tukio kwani hakuna damu iliyokuwa ikitoka kutokana na majeraha waliyoyapata.

Eneo hilo pia halikuwa na ishara ya usumbufu, kuashiria mauaji hayo yalitokea huko, mkuu wa polisi wa Nairobi Adamson Bungei alisema.

Maafisa wa upelelezi wanachunguza mauaji katika tukio hilo. Wanataka kujua ni wapi mwanamke huyo aliuawa.

Mwili huo ulihamishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri uchunguzi wa maiti.

Sababu ya mauaji hayo bado haijajulikana na hakuna mtu aliyekamatwa hadi sasa, polisi walisema.

Wakati huo huo, polisi wanachunguza kisa ambapo mkusanya taka alidungwa na kuuawa katika shambulio la kundi hasimu eneo la Dandora jijini Nairobi.

Dandora ni eneo linalojulika kwa utupaji wa jiji na watozaji wengi hufanya kazi hapo.

Udhibiti wa eneo la kutupa taka ndani ya eneo kubwa ni wa faida na wakati mwingine hubadilika kuwa vurugu na kuua kati ya waendeshaji.

Mnamo Jumatatu, Machi 4, polisi walisema Alex Mwendwa alidungwa kisu na kukimbizwa katika hospitali ya Mama Lucy akiwa na majeraha mengi ambapo alifariki.

Polisi walisema kuwa marehemu alikuwa nyumbani kwa rafiki yake ndani ya Baraka Mowlem walipovamiwa na kundi la wakusanya takataka kutokana na vita vya eneo hilo.

Waathiriwa walizua hofu na mshukiwa mmoja alifukuzwa na kukamatwa na umati ambao ulimpiga kabla ya polisi kumuokoa.

Utafsiri: Samuel Maina