logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Serikali ya Kenya kuiachia miili ya waathiriwa wa Shakahola kwa ajili ya mazishi

Takribani miili 34 imetambuliwa na kuunganishwa na familia zao.

image
na Davis Ojiambo

Habari21 March 2024 - 05:19

Muhtasari


  • • Mackenzie amekana kuhusika na vifo hivyo. Yeye na wafuasi wake kadhaa kwa sasa wanakabiliwa na mashtaka kadhaa, ikiwa ni pamoja na ugaidi, mauaji na mateso.

Serikali ya Kenya inasema kuwa itaiachia baadhi ya miili ya waathiriwa wa ibada ya njaa ya Shakahola wiki ijayo.

Takribani miili 34 imetambuliwa na kuunganishwa na familia zao, kati ya mamia ambayo ilifukuliwa mwaka jana.

Miili ya watu 429 wakiwemo watoto ilifukuliwa kutoka makaburini huko Shakahola, msitu wa mbali nje ya mji wa pwani wa Malindi.

Wengi walionesha dalili za njaa na kushambuliwa. Familia za walionusurika na waathiriwa zilisema, anayejiita kasisi Paul Mackenzie aliwahimiza waumini wa Kanisa lake la Good News International kuhamia huko na kujitayarisha kwa mwisho wa ulimwengu.

Walionusurika wanasema aliwaagiza wafunge ili “wafike mbinguni”.

Serikali itazishauri familia za waathiriwa lakini haitawasaidia kusafirisha miili kwa maziko, alisema mtaalamu mkuu wa serikali Dkt Johansen Oduor Jumatano.

Bw Mackenzie amekana kuhusika na vifo hivyo. Yeye na wafuasi wake kadhaa kwa sasa wanakabiliwa na mashtaka kadhaa, ikiwa ni pamoja na ugaidi, mauaji na mateso.

Uchimbaji mpya umeratibiwa kufanywa baada ya wiki moja hadi mbili,

Dkt Oduor alisema, akiongeza kuwa maeneo 35 zaidi ya makaburi yametambuliwa.

Uchimbaji mpya uliopangwa unaweza kuongeza idadi ya vifo zaidi.

Dkt Oduor alisema kuunganisha miili na familia zao kumekuwa polepole kwa sababu "watu hawafiki kuwachukua wapendwa wao".


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved