Mtandao wa Intaneti wakumbwa na hitilafu kote Afrika Mashariki

Watoa huduma wamesema wanajitahidi kurekebisha tatizo hilo.

Muhtasari

•Watumiaji wa mtandao nchini Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa muunganisho wa intaneti.

•Safaricom, pia nchini Kenya, ilisema "inakabiliwa na changamoto".

Image: BBC

Watumiaji wa mtandao nchini Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa muunganisho wa intaneti huku watoa huduma kote Afrika Mashariki wakikiri kumekuwa na tatizo.

Wamesema wanajitahidi kurekebisha tatizo hilo.

Huduma hiyo ilikumbwa na hitilafu katika nyaya za chini ya bahari zinazounganisha eneo hilo na dunia nzima kupitia Afrika Kusini, mtaalam wa sekta hiyo Ben Roberts aliambia BBC.

Hali kama hiyo ilishuhudiwa katika sehemu za Magharibi na Kusini mwa Afrika mwezi Machi.

Cloudflare Radar, ambayo inafuatilia uunganishaji wa intaneti, imesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathirika zaidi na trafiki kushuka hadi asilimia 30 ya viwango vinavyotarajiwa.

Gazeti la Citizen la Tanzania lilieleza kilichotokea kama "kuzimwa kwa mtandao [ambao] kumeathiri njia kuu za mtandao".

Safaricom, pia nchini Kenya, ilisema "inakabiliwa na changamoto". Airtel Uganda imesema inafahamu kuhusu "huduma ya mtandao ya mara kwa mara".

Na MTN Rwanda ilisema kulikuwa na "suala la uharibifu wa uhusiano wa kimataifa". Malawi, Msumbiji na Madagascar pia zimeathirika kulingana na Cloudflare Radar.

Bw Roberts, kutoka kampuni ya pan-Africa ya Liquid Intelligent Technologies, alisema kuwa amethibitisha kuwa kebo moja inayopitia kando ya pwani ya Afrika Mashariki, inayojulikana kama Eassy, ilikuwa imekatwa mapema Jumapili katika Mji wa bandari wa Afrika wa Durban.

Kebo nyingine pia ilikatwa. Alipuuzilia mbali uwezekano kwamba huenda ni hujuma na uongeza kuha hali kama hiyo wakati mwingine hutokea kwa bahati mbaya.

Kebo zingine zinazounganisha Afrika Mashariki na Ulaya pia zinapatikana na hatua kwa hatua huduma inapaswa kuboreshwa kwani data inapitishwa tena.

Lakini kwa vile makampuni mengi makubwa yana vituo vya data nchini Afrika Kusini uharibifu wa kiungo muhimu ambacho Eassy hutoa ulikuwa na athari kubwa.