EPRA yatangaza bei mpya za mafuta

“Bei hizo ni pamoja na Kodi ya Ongezeko la Thamani ya Asilimia 16 (VAT) kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2023

Muhtasari
  • Katika mapitio ya hivi majuzi bei za mafuta zilizoshuka kwa Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zilipungua kwa Ksh1.00 kwa lita, Ksh1.20 kwa lita na Ksh1.30 kwa lita mtawalia.
Image: BBC

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) imetangaza bei mpya za mafuta kuanza kutumika kuanzia saa sita usiku hadi Juni 14.

Katika mapitio ya hivi majuzi bei za mafuta zilizoshuka kwa Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zilipungua kwa Ksh1.00 kwa lita, Ksh1.20 kwa lita na Ksh1.30 kwa lita mtawalia.

Kufuatia mabadiliko hayo madereva wa magari jijini Nairobi watatozwa Ksh192.84 lita ya petroli, Ksh179.18 kwa dizeli na Ksh168.76 kwa mafuta ya taa.

“Bei hizo ni pamoja na Kodi ya Ongezeko la Thamani ya Asilimia 16 (VAT) kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2023, Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Kodi ya mwaka 2020 na viwango vilivyorekebishwa vya Ushuru wa Bidhaa vilivyorekebishwa kwa mfumuko wa bei kwa mujibu wa Tangazo la Kisheria Na. 194 ya 2020," EPRA ilitangaza.

Katika mapitio hayo, EPRA ilibaini kuwa gharama ya kutua kwa mwagizaji Super Petrol iliongezeka kwa asilimia 3.82 kati ya Machi na Aprili, dizeli ilipungua kwa asilimia 0.46 na Mafuta ya Taa kwa asilimia 0.050 katika kipindi hicho.

Haya yanajiri baada ya kushuka kwa tathmini ya mwisho iliyoshuhudia Wakenya wakilipa Ksh193.84 kwa lita moja ya petroli, Ksh180.38 kwa lita ya dizeli na Ksh170.06 kwa lita moja ya Mafuta ya Taa.