IPOA yaanza uchunguzi baada ya mwanamume,19,kupigwa risasi Kirinyaga

"IPOA, kama ilivyoamrishwa chini ya Sura ya 86 ya sheria za Kenya, imeanza uchunguzi

Muhtasari
  • Wenyeji walifanya vurugu kufuatia ufyatulianaji risasi huo, wakitaka mamlaka ya eneo hilo ipewe maelezo baada ya afisa wa polisi kuhusishwa na tukio hilo.
Mwanafunzi ajiua kwa kujipiga risasi Kilimanjaro
Mwanafunzi ajiua kwa kujipiga risasi Kilimanjaro
Image: YoutubeScreengrab

Mamlaka Huru ya Uangalizi wa Polisi (IPOA) imeanza uchunguzi kuhusu mauaji ya kijana wa miaka 19 katika kituo cha kibiashara cha Kiandai Gichugu, Kaunti ya Kirinyaga.

IPOA katika taarifa ya Jumatatu, Mei 20, 2024, ilisema imeanza uchunguzi kama ilivyoamrishwa chini ya Sura ya 86 ya katiba ya Kenya.

"IPOA, kama ilivyoamrishwa chini ya Sura ya 86 ya sheria za Kenya, imeanza uchunguzi kuhusu mauaji ya kijana katika Kaunti ya Kirinyaga siku ya Jumapili," mamlaka hiyo ilisema.

Wenyeji walifanya vurugu kufuatia ufyatulianaji risasi huo, wakitaka mamlaka ya eneo hilo ipewe maelezo baada ya afisa wa polisi kuhusishwa na tukio hilo.

Derrick Gachoki aliuawa kwa kupigwa risasi saa kumi na mbili jioni wakati maafisa wa polisi waliokuwa wakishika doria walipofika katika kituo cha soko.