Sonko amuonya mwanablogu Maverick dhidi ya kumchafulia jina

Sonko alilazimika kueleza ukweli kuhusu maisha ya bintiye aliye ng’ambo baada ya mwanablogu huyo kuchapisha madai kuhusu mabinti

Muhtasari

•Sonko pia alikanusha madai ya Aoko kwamba Anne Mvurya ambaye ni rafiki wake (Sonko) wa karibu, ameavya mimba zake baada ya madai ya kuwa na uhusiano na Gavana huyo wa zamani.

MIKE SONKO
MIKE SONKO
Image: Screengrab

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko siku ya Jumanne alimuonya mwanablogu mwenye utata, Maverick Aoko kuhusu machapisho yake yanayodaiwa kumchafulia jina kwenye mitandao ya kijamii.

Sonko alilazimika kueleza ukweli kuhusu maisha ya bintiye aliye ng’ambo baada ya mwanablogu huyo kuchapisha madai kuhusu mabinti zake Gavana huyo wa zamani na kiongozi wa zamani wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi, Anne Mvurya ambaye ni mshirika wa karibu wa Sonko.

Katika chapisho refu kwenye akaunti yake ya X (zamani twitter), Sonko alifafanua madai hayo na hata akachapisha stakabadhi za masomo za bintiye, Sandra Mbuvi ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Brighton International College nchini Uingereza, na kupuuzilia mbali madai ya Aoko kuhusu masomo ya bintiye.

Aoko alidai kuwa Sandra anajihusisha na shughuli haramu nchini Uingereza badala ya kuelekeza nguvu zake katika masomo.

"Ikiwa binti yangu alikuwa akijihusisha na shughuli ulizodai, hangekuwa anaomba pesa za matumizi kutoka kwangu kila wiki. Kama Baba anayewajibika, mimi binafsi huongeza kadi yake ya benki kati ya Shilingi 60,000 hadi 100,000 kila wiki. Hangefaulu mitihani yake kwa kishindo ili kuhitimu hadi ngazi ya juu ya taaluma yake,” Sonko alisema.

Sonko pia alikanusha madai ya Aoko kwamba Anne Mvurya ambaye ni rafiki wake (Sonko) wa karibu, ameavya mimba zake baada ya madai ya kuwa na uhusiano na Gavana huyo wa zamani.

“Ili kuthibitisha kuwa umekosea, Ann Mvuria, alijifungua mtoto wa kiume ambaye ana umri wa miaka miwili sasa. Nimuingiza katika Shule ya Sheria ya Kenya, ambapo alihitimu hivi majuzi na kuwekwa kilemba cha uwakili. Leo, yuko katika jopo la mawakili wanaoniwakilisha mahakamani,” aliongeza Sonko.

Sonko hata hivyo hakufafanua kama yeye ndiye baba wa mtoto wa Mvurya.

Aoko alichapisha madai hayo kwenye akaunti yake ya X baada ya Sonko kumtaja kama a "“dirty woman”" katika mahojiano ya moja kwa moja ya YouTube na mcheshi wa TV, Obinna.