Donald Trump akana kuwa na hatia yoyote

Trump asema uamuzi wa jaji haukuawa huru na haki

Muhtasari

•Uamuzi huu ulikuwa wa fedheha na sio wa huru na haki.

•Uamuzi halisi utaamuliwa tarehe 5 Novemba na watu. 

Trump akiwa kortini
Image: BBC

Trump amekana mashtaka yaliyowekwa dhidi yake kwa kusema kuwa ilikuwa ni njama ya mpinzani wake Joe Biden ya kuhakikisha kuwa hayupo debeni kwenye kindubwendubwe  kikali cha uchaguzi wa mwaka huu Marekani.

Mahakama jana ilimpataTrump na hatia ya makosa ya jinai ambapo alishtakiwa kutokana na kujihusisha kwa uhalifu wa karibu makosa thelathini na manne. Makosa hayo yanahusisha udanganyifu wa rekodi za kibiashara baada ya kumlipa mburudishaji Stormy Daniels dola 130,000 kabla ya uchaguzi. Akizungumza Trump alikuwa na haya ya kusema:

"Uamuzi huu ulikuwa wa fedheha na sio wa huru na haki. Huu ulikuwa mtihani uliopangwa na jaji aliye na mgongano wa maslahi na adui wa taifa letu."

"Hatupati mabadiliko ya eneo, tuko kwenye asilimia tano au sita katika eneo hili.Uamuzi halisi utaamuliwa tarehe 5 Novemba na watu na wanajua kilichotokea hapa na kila mtu anajua kilichofanyika papa hapa.''

''Hatukufanya chochote, mimi ni mtu asiye na hatia ila ni sawa, ninapigania nchi yetu, ninapigania katiba yetu. Nchi yetu nzima inapangwa."

"Mambo yote haya yalifanywa na utawala wa Biden ambaye ni adui mkuu wa Demokrasia ya Amerika."

Fauka ya hayo, Trump aliandika haya kwenye ukurasa wake wa  X ama Twitter akiwa na haya ya kusema, ''Haki zangu za kiraia zimevunjwa kabisa na uwindaji haramu kwenye siasa kali, usio na katiba, na kuingilia kati uchaguzi ambapo taifa letu linayumba na kuchekwa kote ulimwenguni."

Baraza la waamuzi lilifikia uamuzi huo baada ya masaa tisa ya mashauriano. Hakimu Juan Merchan aliwaongoza waamuzi hao kwa muda wa saa moja, wakiangazia mashtaka thelathini ya udanganyifu na ulaghai dhidi ya Trump.

Ushahidi ulioletwa mbele ya baraza hilo ulijumuisha tetesi za njama za kuficha malipo hayo kuenda Kwa mburudishaji Stormy Daniels.

Donald Trump vilevile anazo kesi tatu zinazomkabili dhidi yake ikiwemo, kesi ya kuingilia uchaguzi wa shirikisho pale mjini wa Washington DC, kuingilia uchaguzi katika eneo la Georgia na vilevile kesi kutoka kwa shirikisho kuwa alicheza na hati za maana za taifa na pia ujumbe unaohusisha usalama wa taifa.

Hukumu itafanyika mnamo tarehe kumi na mmoja mwezi wa Julai mwaka huu