Wakenya wengi wapinga mswada wa kifedha wa mwaka 2024

Gharama kubwa ya maisha na ushuru mkubwa ndio mojawapo ya sababu za wengi kuamini tafa linaelekea pabaya

Muhtasari

•Wahojiwa walitaja utaratibu wa kodi pamoja na gharama kubwa ya maisha nchini unafanya taifa lielekee pabaya.

•Asilimia 19 ya waliohojiwa walikubali kuwa nchi iko kwenye njia sahihi. 

•Tofauti ya kikanda unasisitiza hitaji ya serikali kutekeleza sera zinazolengwa ipasavyo.

Wakenya waandamana dhidi ya utozaji mkubwa wa ushuru
Image: BBC

Wakenya wengi wamepinga mpango wa ushuru wa Rais William Ruto huku nchi ikijiandaa kuangazia Mswada wa Fedha wa 2024 unaoelezea hatua za kukusanya ushuru.

Katika kura mpya ya maoni iliyotolewa Alhamisi na shirika la Infotrack , wakenya wengi walikuwa na maoni kuwa nchi inaelekea pabaya wakitaja sera ya kuhusu ushuru kama ilivyopendekezwa katika Mswada wa Fedha wa mwaka 2024.

Utafiti wa Infotrak unaonyesha kuwa, asilimia 63 ya wakenya hawajafurahishwa na mwelekeo ambao nchi imechukua. Walipoambiwa waeleze sababu za maoni yao, wahojiwa walitaja utaratibu wa kodi pamoja na gharama kubwa ya maisha nchini.

Miongoni mwa sababu zilizotajwa kwamba nchi inaelekea katika mwelekeo mbaya, ni pamoja na kuwa na gharama kubwa ya maisha (asilimia 45) na ushuru mkubwa kwao (asilimia 27)," ripoti hiyo inaonyesha.

Vilevile, utafiti huo ulifanywa kati ya Mei 23 na 29, 2024. Jumla ya wahojiwa 1,700 walihojiwa kutoka kaunti zote 47 ili kuhakikisha uwakilishi wa kitaifa.

Kutokana na kura ya maoni, asilimia 19, ndogo ya waliohojiwa walikubali kuwa nchi iko kwenye njia sahihi. Jambo la kustaajabisha ni kwamba, zaidi ya nusu ya waja waliohojiwa kutoka maeneo ya Kati na Bonde la Ufa waliamini kuwa nchi inaelekea pabaya.

Katika eneo la Bonde la Ufa—upande wa nguvu wa rais Ruto—asilimia 54 walisema nchi iko kwenye njia mbaya. Katika uwanja wa kati wa Naibu Rais Rigathi Gachagua, kiwango cha kutoidhinishwa kilipanda hadi asilimia 63.

Kutokana na matokeo hayo, Nairobi inaongoza kwa asilimia 74 ya watu ambao wana maoni kuwa nchi iko kwenye njia mbaya inayofuatwa na eneo la Mashariki. Asilimia 68 ya wahojiwa kutoka Nyanza walisema nchi haiko katika mwelekeo sahihi, Magharibi (asilimia 64), Pwani (asilimia 61) na Kaskazini Mashariki (asilimia 47).

Utafiti ulikuwa na asilimia 2.53 ya kiwango cha makosa na asilimia 95 ya kiwango cha kujiamini. Utafiti huo ambao ulitolewa Alhamisi pia unaonyesha kuongezeka kwa uelewaji kuhusu Mswada wa Fedha huku asilimia 54 wakisema wanaufahamu.

Muswada wa sheria wa Fedha unaelezea jinsi serikali inakusudia kupata pesa kufadhili bajeti. "Wengi wa waliohojiwa katika eneo la kati, asilimia 62, wanafahamu Muswada wa Sheria wa Fedha wa 2024, tofauti na mikoa mingine ya Mashariki (asilimia 41), ambayo ilipata alama ndogo zaidi katika ufahamu wa Mswada huo. Hata hivyo, iliibuka ya pili kwa (asilimia 59) kwa ufahamu,” ripoti hiyo inaonyesha.

"Hii ni dalili tosha ya kiwango cha uhamasishaji na elimu kinachoendelea katika mikoa kuhusu Muswada huo."

Kutokana na utafiti huo, wakenya walieleza gharama ya maisha na ajira iliyokuwa na wasiwasi mkuu katika asilimia 49 na asilimia 30 mtawalia.

"Gharama ya maisha na ukosefu wa ajira yamekuwa masuala yanayosumbua mara kwa mara katika kura za maoni za hivi majuzi zilizofanywa tangu Agosti/Septemba 2023 na Februari 2024," ripoti hiyo yasema.

"Mkoa wa Nyanza uliibuka kwa kiwango cha juu zaidi (asilimia 60) kulingana na Wakenya ambao walitambua gharama ya maisha kuwa jambo la msingi." 

“Mikoa mingine, ikiwa ni pamoja na Pwani, Kaskazini Mashariki, Nairobi, Kati, Bonde la Ufa, Magharibi na Mashariki ilipata alama za chini ya wastani kulingana na gharama ya maisha. Tofauti hii ya kikanda inasisitiza hitaji la sera zinazolengwa kutekelezwa ipasavyo.