Tunatishwa katika ofisi ya Uhuru - Kanze Dena

Akizungumza wakati wa kikao na wanahabari, Kanze alisema serikali pia imekataa kuwaongezea kandarasi wafanyakazi wawili.

Muhtasari
  • "Kuna uondoaji usio wa kawaida na vitisho vya wafanyikazi kupitia simu usiku wa manane," anasema.
State House, KWA HISANI
State House, KWA HISANI
Image: Kanze Dena

Msemaji Kanze Dena ameripoti vitisho vya wafanyikazi na simu za usiku katika afisi ya Ofisi ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta.

"Kuna uondoaji usio wa kawaida na vitisho vya wafanyikazi kupitia simu usiku wa manane," anasema.

Akizungumza wakati wa kikao na wanahabari, Kanze alisema serikali pia imekataa kuwaongezea kandarasi wafanyakazi wawili.

Wafanyakazi aliosema ni Kanze Dena Mararo na msimamizi John Kariuki.

"Ofisi bado inasubiri uthibitisho na mawasiliano juu ya kwa nini walikataa kwa uwazi kuorodhesha kandarasi za wafanyikazi hawa wawili wa kitaalam," alisema.

Aidha alisema serikali haijafanya wala kuwezesha ukarabati wowote, matengenezo ya gari lolote wala haijatumia mafuta ya gari chini ya ofisi hii.

Katika kikao na wanahabari, Uhuru kupitia kwa msemaji wake Kanze Dena badala yake alisema kwa sasa anatumia magari aliyopewa kwa njia ya mpito.

Kanze alisema magari yanayotumika ni yale ambayo Uhuru aliondoka nayo kutoka Kasarani baada ya hafla ya kukabidhi MAMLAKA mnamo Septemba 2022.

"Baada ya mabadiliko hayo, mazungumzo kuhusu ununuzi wa magari hayo kama inavyotakiwa na Sheria yalianza kati ya ofisi hizo mbili...," Kanze alisema.