Mwanasiasa mkongwe Maina Wanjigi aaga dunia

Wanjingi alifariki akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi akiwa na umri wa miaka 92.

Muhtasari

• Maina Wanjigi na babake mwanasiasa na mfanyibiashara Jimmy Wanjigi.

Maina Wanjigi
Maina Wanjigi

Mwanasiasa mkongwe Maina Wanjigi ameaga dunia.

Wanjingi alifariki akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi akiwa na umri wa miaka 92.

Maina Wanjigi na babake mwanasiasa na mfanyibiashara Jimmy Wanjigi.

Wanjingi alihudumu kama mbunge kwa zaidi ya miaka 25 na alishika wa uwaziri katika wizara mbali mbali kama vile Kilimo, Ujenzi na Utalii.

Wakati wa enzi za rais wa kwanza Jomo Kenyatta, Maina alihusika katika kuwapa makao maelfu ya raia wasio na ardhi katika nafasi yake kama Mkurugenzi wa Makazi.

Alijiunga na siasa mnamo Novemba 1969 katika uchaguzi mdogo wa Kamukunji ambao ulisababishwa na mauaji ya Tom Mboya.

Pia alihudumu katika utawala wa rais wa zamani Daniel Moi alipoteuliwa kama mwenyekiti wa shirika la ndege la Kenya Airways mwaka wa 1979 kabla ya kuteuliwa waziri wa Utalii na Wanyamapori miaka minne baadaye.

Mnamo 1990, alifukuzwa kutoka chama kilichokuwa tawala wakati huo KANU kwa kutetea siasa za vyama vingi. Baada ya hapo, alikamatwa, kuhojiwa na kushikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Lang’ata kwa siku tatu kabla ya kufikishwa mahakamani lakini hakuna mashtaka yaliyopendekezwa dhidi yake.

Maina aliingia siasa za Upinzani na kujiunga na mrengo wa Ford Asili wa Kenneth Matiba ambapo walijaribu bila mafanikio kumwondoa Moi mamlakani katika Uchaguzi Mkuu wa 1992.