Waandamanaji wapanga zaidi ya majeneza 10 CBD Nairobi

Waliposogea mbali na polisi, walibeba majeneza huku wakiwa wameyafunika kwa Bendera za Kenya.

Muhtasari
  • Waandamanaji walionekana wakiwa wamebeba majeneza hayowalipokuwa wakiyapanga eneo la CBD.
Image: SCREENGRAB

Waandamanaji Jumanne walijitokeza na zaidi ya majeneza 10 katika Wilaya ya Biashara ya Kati ya Nairobi.

Waandamanaji walionekana wakiwa wamebeba majeneza hayowalipokuwa wakiyapanga eneo la CBD.

Waliposogea mbali na polisi, walibeba majeneza  huku wakiwa wameyafunika kwa Bendera za Kenya.

Baadhi ya maafisa walionekana wakiondoa masanduku hayo huku waandamanaji wakiyarudisha barabarani.

Wengine walitangulia kufungua kasha huku wakipambana na polisi waliokuwa wakirusha mabomu ya machozi kuwatawanya vijana hao.

Ni maandamano ambayo yameingia wiki ya tatu huku Gen Z wakipinga mswada wa fedha.

Waandamanaji mjini Mombasa wameweza kuteketeza gari.

Mengi yafuata;