Orodha ya hatua ambazo Rais Ruto ametoa kupunguza matumizi ya serikali

Rais ametangaza hatua kadhaa ambazo serikali yake itachukua ili kupunguza matumizi ya fedha za serikali.

Muhtasari

•Ruto alifanya matangazo hayo wakati wa hotuba yake ya siku ya Ijumaa katika ikulu kuu ya Nairobi.

RAIS WILLIAM RUTO
Image: PCS

Rais William Ruto ametangaza hatua kadhaa ambazo serikali yake itachukua ili kupunguza matumizi ya fedha za serikali.

Ruto alifanya matangazo hayo wakati wa hotuba yake ya siku ya Ijumaa katika ikulu kuu ya Nairobi.

Katika hotuba yake, alisema kufuatia mashauriano mapana wameafikiana kupunguza gharama mbalimbali zikiwemo;

Kufunga angalau mashirika 47 ya serikali yenye huduma zinazoambatana.ii) Kusimamishwa kazi kwa Makatibu Tawala Wakuu (CAS).

iii) Kupunguza washauri serikalini kwa angalau asilimia 50 mara moja.

iv) Kuondoa Bajeti katika Ofisi za Mke wa Rais, Mke wa Naibu Rais na Mke wa Waziri Mkuu.

v) Bajeti za siri katika Ofisi ya Urais pia zimeondolewa.

vi) Bajeti ya ukarabati serikalini itapunguzwa kwa asilimia 50.

vii) Watumishi wa Umma watakaofikisha umri wa miaka 60 watatakiwa kustaafu mara moja na hakuna nyongeza itakayoruhusiwa.

viii) Kusimamisha ununuzi wa magari mapya serikalini kwa mwaka mmoja, isipokuwa kwa vyombo vya ulinzi na usalama.

ix) Usafiri wote usio wa lazima wa maafisa wa serikali pia umesitishwa.

x) Hakuna afisa wa serikali au mtumishi wa umma atakayeshiriki katika Harambee.