Rais Ruto awaagiza maafisa wa serikali na wafanyikazi wa umma kutoshiriki harambee

Rais alitoa agizo hilo katika hotuba yake ya Ijumaa alasiri katika ikulu ya Nairobi.

Muhtasari

•Alimwelekeza mwanasheria mkuu wa serikali kutengeneza njia mbadala ya michango ya hisani kwa umma.

Image: screengrab

Rais William Ruto amepiga marufuku maafisa wote wa serikali na wafanyikazi wa umma kushiriki kwenye michango ya umma na harambee.

Rais alitoa agizo hilo katika hotuba yake ya Ijumaa alasiri katika ikulu ya Nairobi.

Alimwelekeza mwanasheria mkuu wa serikali kutengeneza njia mbadala ya michango ya hisani kwa umma.

"Hakuna afisa wa serikali au mtumishi wa umma atakayeshiriki katika michango au harambee za umma kuendelea," rais William Ruto aliagiza.

Aliongeza, "Mwanasheria mkuu anaagizwa kutayarisha na kuwasilisha usajili kwa njia hii na kuwasilisha sheria  na kuwasilisha utaratibu ulioandaliwa wa michango iliyopangwa ya uwazi kwa madhumuni ya umma, hisani na uhisani."