logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Serikali yashinikizwa kuhakikisha wanajeshi wa zamani wanaishi maisha mazuri

Waligawa vyakula vya aina mbalimbali kwa familia za wenzao waliokufa wakiwa kazini ili kuwahudumia katika nyakati ngumu za kiuchumi.

image
na SAMUEL MAINA

Habari07 July 2024 - 12:08

Muhtasari


  • •Waligawa vyakula vya aina mbalimbali kwa familia za wenzao waliokufa wakiwa kazini ili kuwahudumia katika nyakati ngumu za kiuchumi.
walitoa usaidizi kwa wanajeshi wastaafu wenzao.

Maafisa wastaafu wa jeshi la ulinzi la kenya chini ya mwavuli (Kenya Veterans for Peace) wameitaka serikali kuingilia kati na kuhakikisha wanajeshi wa zamani wa KDF wanaishi maisha ya starehe.

Akizungumza alipowatembelea Wanajeshi wa zamani wa KDF,  Afisa Mkuu Mtendaji  wa Veterans  For Peace, Dkt Nelson Sechere alisema Wanajeshi hao wa Zamani walitumikia nchi kwa bidii na hawafai kusahaulika.

Maveterani hao walitoa usaidizi kwa wenzao waliostaafu na familia za maafisa waliofariki katika kaunti ya Machakos.

Waligawa vyakula vya aina mbalimbali kwa familia za wenzao waliokufa wakiwa kazini ili kuwahudumia katika nyakati ngumu za kiuchumi.

Dkt Sechere alisema wanalenga maeneo yote, na pia wanachimba visima kadhaa ili kuchangia usalama wa chakula nchini.

Luteni kanali mstaafu Moses Sande, mnufaika wa mpango wa chakula anasema waliunda shirika hilo baada ya ghasia za baada ya uchaguzi wa 2008 ili kutetea amani miongoni mwa jamii tofauti.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved