logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rais Ruto amuomboleza Kasisi Allan Kiuna

Kiuna alifariki kutokana na saratani ya myeloma kwa mara ya kwanza mwaka wa 2018/2019.

image
na Davis Ojiambo

Habari10 July 2024 - 09:17

Muhtasari


  • •"Kwa mkewe, Mchungaji Kathy Kiuna na familia tunasimama nawe katika wakati huu wa huzuni na maombolezo, na tunakuombea upate ujasiri wa kustahimili kipindi hiki cha majaribu." Aliandika Rais Ruto
  • •Kiuna alifariki kutokana na saratani ambapo alipatikana na saratani ya myeloma kwa mara ya kwanza mwaka wa 2018/2019.

Rais William Ruto ameungana na Wakenya wengine na waumini wa kanisa la Jubilee (JCC) katika kumuomboleza mhubiri Allan Kiuna.

Akitumia jukwaa lake la X, rais alitoa ujumbe wake wa rambi rambi akiwa na haya ya kusema:

"Ni kwa masikitiko makubwa nilipopata habari za kifo cha Askofu Allan Kiuna.

Ninaungana na jumuiya ya Wakristo kuomboleza kifo chake. Askofu Kiuna alikuwa kiongozi wa Kikristo aliyejitolea ambaye alianzisha Kanisa la Kikristo la Jubilee (JCC) na kuwatia moyo wengi kufuata mafundisho ya Bwana.

Kwa mkewe, Mchungaji Kathy Kiuna na familia tunasimama nawe katika wakati huu wa huzuni na maombolezo, na tunakuombea upate ujasiri wa kustahimili kipindi hiki cha majaribu.

Apumzike kwa amani.'' alimalizia ujumbe huo Rais Ruto.

Allan Kiuna alikuwa mchungaji mashuhuri kutoka kanisa la Jubilee Christian Church.Kiuna alifariki kutokana na saratani ambapo alipatikana na saratani ya myeloma kwa mara ya kwanza mwaka wa 2018/2019.

Mnamo mwaka wa 2019, Kiuna alishiriki mapambano yake ya saratani na umma, akimshukuru Mungu kwa kumuona katika jaribu hilo gumu.

Kiuna alipatiwa matibabu nchini Marekani kwa mwaka mmoja, ambayo iligharimu takriban dola milioni 3 (takriban Sh460 milioni).

Licha ya mzigo huo wa kifedha, alimshukuru Mungu kwa kumjalia wakati huo.

Mapema 2023, Kiuna alirejea nyumbani bila saratani, akisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 57 na maadhimisho ya miaka 29 ya wanandoa hao.

Hata hivyo, haijafahamika ni lini saratani hiyo ilirejea tena na hivyo kusababisha kifo chake ambapo wananchi walifahamishwa hapo jana.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved