Faith Kipyegon, Moraa wawasili Paris kwa michezo ya Olimpiki

Hafla hizo zimepangwa kuanza rasmi Agosti 1-11.

Muhtasari
  • Kipyegon atakuwa akitafuta kupata dhahabu yake ya tatu mfululizo ya Olimpiki katika fainali ya mita 5,000 kwa wanawake mnamo Agosti 5.
Image: TEAM KENYA/ X

Ikiwa imesalia siku moja tu kuanza kwa mashindano ya riadha katika michezo ya Olimpiki ya Paris inayoendelea, timu ya wanariadha wa Kenya kushiriki katika michezo hiyo imewasili nchini.

Hafla hizo zimepangwa kuanza rasmi Agosti 1-11.

Timu hiyo inayoongozwa na mshindi mara tatu wa medali ya dhahabu katika Olimpiki na nahodha Faith Kipyegon waliwasili Jumanne asubuhi kabla ya kuelekea katika kijiji cha Olimpiki wanakoishi.

Aliandamana na Mary Moraa, Timothy Cheruiyot, Brian Komen, Beatrice Chebet, Bernard Kibet na Lilian Odira.

Wengine ni Vivian Chebet, Reynold Cheruiyot, Margaret Chelimo, Daniel Mateiko na Nicholas Kimeli.

Kuna matukio 48 yanayojumuisha 23 kila moja kwa wanaume na wanawake na vile vile matukio mawili mchanganyiko-4x400m relay na 35km mchanganyiko wa mbio za timu.

Itafanyika katika uwanja wa Stade de France jijini Paris.

Maeneo matatu yameandaliwa kwa ajili ya matukio ya barabarani ambayo ni Hotel de Ville na Led Invalides kwa ajili ya kuanza na kumaliza mbio za marathon na Pont d’lena kwa matembezi ya mbio.

Kipyegon atakuwa akitafuta kupata dhahabu yake ya tatu mfululizo ya Olimpiki katika fainali ya mita 5,000 kwa wanawake mnamo Agosti 5.

Atashiriki katika raundi ya kwanza ya mita 1,500 mnamo Agosti 6.

Isipotee kwamba hakuna mwanariadha wa Kiafrika aliyewahi kushinda dhahabu katika mashindano hayo mara tatu mfululizo.

Mwanariadha wa mbio za marathoni Eliud Kipchoge pia atajiandaa kwa pambano kuu na Kenenisa Bekele.

Fainali ya mita 10,000 kwa wanaume imepangwa kufanyika Ijumaa.

Daniel Mateiko, Bernard Kibet na Nicholas Kimeli watakuwa nje kunyakua taji lililonyakuliwa mara ya mwisho na John Ngugi wakati wa Olimpiki ya Seoul 1998 watakapokutana na Jacob Kiplimo na Joshua Cheptegei kutoka Uganda.

Cheruiyot atashiriki katika nusu-fainali ya mita 1,500 wanaume mnamo Agosti 4.

Moraa kwa upande wake atashiriki Agosti 2 kwa raundi ya kwanza ya mita 800.