logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mbunge Oscar Sudi ajishaua kuvaa saa ya milioni 16

" Zilikuwa mbili na hata sikuwahi jua zilikuwa zinagharimu hela ngapi,” alisema Oscar Sudi.

image
na Samuel Maina

Habari02 August 2024 - 08:32

Muhtasari


  • •" Zilikuwa mbili na hata sikuwahi jua zilikuwa zinagharimu hela ngapi,” alisema Oscar Sudi.
  • •Baadhi ya viongozi wengi nchini Kenya wamekuwa wakijipiga kifua kuhusiana na utajiri wanaomiliki.
Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi amewaduwaza wakenya wengi baada ya kujishaua kwa madaha na madoido kuhusiana na saa aliyoivaa ambayo alisema iligharimu takriban milioni 16 na zaidi.

Haya yanajiri huku baadhi ya wakenya wakishangaa kupindukia namna kiongozi huyo anaweza kujipamba na saa hiyo mkononi wakati taifa linakumbwa na masaibu mengi hasa ya kiuchumi.

Akizungumza kwenye idhaa ya Obinna Show, alieleza namna alivyopata saa hiyo.

“Nilipatiwa saa hiyo na aliyekuwa waziri mkuu wa zamani wan chi nyingine. Zilikuwa mbili na hata sikuwahi jua zilikuwa zinagharimu hela ngapi,” alisema Oscar Sudi.

“ Wakati mwingine wakenya wako kwenye upande mbaya. Saa hii haikuundiwa miti wala ng’ombe bali iliundiwa binadamu. Mnataka nani wavae saa hii? Tuache kuwa na tamaa na gere,” aliongeza.

Hali hii iliibua msisimuko mkali miongoni mwa wakenya mitandaoni huku wengi wakiwa wamejawa na ghadhabu na hamaki.

“Ati prime minister? Huo ni ushuru wetu,” aliandika 5star Nick Kwenye Instagram.

“Sisi si wajinga!” Alidokeza young brian.

“Hata Ruto alizawadiwa ndege ya milioni 200 kuelekea Marekani,” aliandikisha Hamolitz huku akiangua kicheko.

“Tafakari kuwa kwenye taifa ambapo mshahara mdog ni chini ya dola kasha unazungumza kuhusu saa ya shilingi milioni 17. Wakenya wengi wanaumia; wagonjwa wangu wengi wanaaga kutokana na kukosa 1/20 ya saa hii,” alisema daktari Japrado mtandaoni.

Yakini, baadhi ya viongozi wengi nchini Kenya wamekuwa wakijipiga kifua kuhusiana na utajiri wanaomiliki.

Hapo awali, aliyekuwa waziri mkuu wa barabara bwana Kipchumba Murkomen alikuwa hewani ambapo pia aliwabung’aza wengi baada ya kuambia wananchi kuwa anavaa saa ya shilingi laki tisa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved