Odinga awasili Elgeyo Marakwet kwa mazishi ya Mzee Chirchir Masit

Mzee Chirchir Masit ni babake aliyekuwa Kamishna wa IEBC Irene Masitt aliye uhamishoni.

Muhtasari

• Masit alikuwa mmoja wa makamishna wanne wa IEBC waliokataa matokeo ya uchaguzi uliopita na huku wengine wakijiuzulu baadaye alikataa kufanya hivyo.

Kinara wa ODM Raila Odinga akwasili kwa mazishi ya Mzee Chirchir Masit, marehemu ni babake aliyekuwa kamishna wa IEBC Irene Masit /13 Agosti 2024.
Kinara wa ODM Raila Odinga akwasili kwa mazishi ya Mzee Chirchir Masit, marehemu ni babake aliyekuwa kamishna wa IEBC Irene Masit /13 Agosti 2024.
Image: MATHEWS NDANYI

Kiongozi wa ODM Raila Odinga amewasili Elgeyo Marakwet kuhudhuria mazishi ya Mzee Chirchir Masit ambaye ni babake aliyekuwa Kamishna wa IEBC Irene Masitt aliye uhamishoni.

Mzee Masit atazikwa leo (Jumanne) huko Chepkorio ambapo ibada ya wafu inaendelea.

Atazikwa bila bintiye ambaye bado yuko nje ya nchi baada ya kutoroka kwa hofu ya usalama wake.

Masit alikuwa mmoja wa makamishna wanne wa IEBC waliokataa matokeo ya uchaguzi uliopita na huku wengine wakijiuzulu baadaye alikataa kufanya hivyo.

Kinara wa ODM Raila Odinga na mbunge wa Kapseret Oscar Sudi.
Image: MATHEWS NDANYI

Hata hivyo baadaye aliondolewa afisini kufuatia mapendekezo ya jopo lililoundwa kumchunguza.

Raila anahudhuria pamoja na Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi na gavana wa eneo hilo Wisley Rotich miongoni mwa viongozi wengine.

Viongozi wengine kadhaa wa kisiasa pia wanatarajiwa kuhudhuria.

IMETAFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO