• Mafuta ya petroli yatauzwa kwa Sh188.84, dizeli Sh171.60 huku mafuta taa yakiuzwa kwa Sh161.75 jijini Nairobi kuanzia saa sita usiku.
Bei ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta taa itasalia vile ilivyo kwa kipindi cha mwezi mmoja ujao.
Mamlaka ya Udhibiti wa kawi na Petroli nchini Kenya (Epra) siku ya Jumatano ilitangaza bei za mafuta kuanzia tarehe 15 Agosti 2024 hadi Septemba 14, 2024.
Bei za mafuta zimesalia bila kubadilika katika tangazo jipya la bei za bidhaa hiyo muhimu.
Mafuta ya petroli yatauzwa kwa Sh188.84, dizeli Sh171.60 huku mafuta taa yakiuzwa kwa Sh161.75 jijini Nairobi kuanzia saa sita usiku.
“Kwa mujibu wa Kifungu cha 101(y) cha Sheria ya Petroli ya mwaka 2019 na notisi ya kisheria nambari 192 ya mwaka 2022, hatujabadilisha bei za juu zaidi za rejareja za mafuta ya petroli, ambazo zitaanza kutumika kuanzia Agosti 15, 2024 hadi Septemba 14, 2024. ," Epra ilisema katika taarifa.
"Katika kipindi kinachoangaziwa, bei ya juu inayoruhusiwa ya petroli, dizeli na mafuta ya taa bado haijabadilika."
Epra ilisema kuwa bei hizo ni pamoja na kodi ya Ongezeko la Thamani ya asilimia 16 (VAT) kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Fedha ya 2023, Sheria ya Kodi ya Sheria ya 2020 na viwango vilivyorekebishwa vya Ushuru wa bidhaa.