logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mpox sio kama covid inaweza kudhibitiwa - Mtaalamu

Virusi vipya vya maambukizi haya, Clade Ib, vimethibitishwa nchini Uswidi wiki iliyopita.

image
na Davis Ojiambo

Habari21 August 2024 - 06:24

Muhtasari


  • • Virusi hivyo vinavyosababisha homa na upele vinaweza kusambazwa kwa kugusana na ngozi na vidonda, ikiwa ni pamoja na wakati wa kujamiiana.

Homa ya nyani yaani Mpox "sio Covid mpya", kwa sababu mamlaka zinajua wazi jinsi ya kudhibiti kuenea kwake, mtaalam mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni amesema.

Licha ya wasiwasi kuhusu aina mpya ya virusi, na tahadhari ya kimataifa, mkurugenzi wa kanda ya Ulaya Dk Hans Kluge amewaambia waandishi wa habari, pamoja tunaweza – na ni lazima - kukabiliana na mpox.

Na hatua madhubuti lazima ichukuliwe sasa hivi - ikiwa ni pamoja na kuhakikisha chanjo zinafika maeneo yenye uhitaji mkubwa – hiyo inaweza kukomesha mzunguko mwingine wa hofu.

Virusi vipya vya maambukizi haya, Clade Ib, vimethibitishwa nchini Uswidi wiki iliyopita na kuhusishwa na mlipuko unaoongezeka barani Afrika.

Mpox imeua takriban watu 450 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, iliyojulikana zamani kama Zaire, katika miezi ya hivi karibuni, ikiwa ni yenye kuhusishwa na virusi Clade Ib.

Bado kuna mengi ya kujifunza kuhusu kirusi kipya, wataalam wanasema, lakini vinaweza kuenea kwa urahisi na kusababisha ugonjwa mbaya zaidi.

Virusi hivyo vinavyosababisha homa na upele vinaweza kusambazwa kwa kugusana na ngozi na vidonda, ikiwa ni pamoja na wakati wa kujamiiana.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved