Kenya yathibitisha mgonjwa wa pili wa Mpox

Dereva huyo alifanyikwa uchunguzi katika mji wa mpakani wa Busia magharibi mwa Kenya.

Muhtasari

•Mwanamume ambaye ni dereva wa lori mwenye historia ya kusafiri kutoka D.R.C. amepatikana na virusi vya Homa ya Nyani au Mpox.

Image: BBC

Wizara ya afya ya Kenya inasema mwanamume ambaye ni dereva wa lori mwenye historia ya kusafiri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (D.R.C.) amepatikana na virusi vya Homa ya Nyani au Mpox.

Dereva huyo alifanyikwa uchunguzi katika mji wa mpakani wa Busia magharibi mwa Kenya.

Sampuli yake ilithibitishwa kuwa na virusi katika uchubguzi wa maabara. Mtu huyo kwa sasa ametengwa na yuko chini ya uangalizi wa karibu.

Aidha uchunguzi wa kina wa watu wanaoshukiwa kuwa na virusi vya Mpox umeimarishwa katika eneo hilo na katika kaunti zote ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.