Kamati za kutathimini mfumo wa ufadhili wa masomo ya vyuo vikuu yaundwa

Tishio la mgomo ya wahadhiri na migomo ya awali ya wanafunzi yapelekea Rais kubuni Kmati maalum

Muhtasari

• Rais Ruto ameteua kamati ya kuangazia elimu ya vyuo vikuu baada ya malalamishi ya wanafunzi kupitia migomo na tishio la wahadhiri kuandaa mgomo.

• Kamati hiyo imejengwa kwa msingi ya kamati nne kuu zitakazoshughulikia maswala tofauti tofauti.

Rais William Ruto
Rais Ruto Rais William Ruto
Image: PCS

Rais Dkt. William Ruto ameteua kamati ya kutathmini mfumo mpya wa ufadhili wa masomo ya vyuo vikuu.

Kamati hiyo imeundwa kwa misingi ya kamati nne ndogo ambazo ni kamati za kuboresha mfumo mpya wa ufadhili wa vyuo vikuu na taasisi, kamati ya kuangazia rufaa zinazotokana na malalamishi ya uainishaji wa wanafunzi katika vitengo vya ufadhili, kamati ya kuunda mikopo ya wanafunzi na kamati ya kuangazia gharama ya programu za kitaaluma za vyuo vikuu.Mathew Rotich na Joseph Musyoki watahudumu kama makatibu chini ya Agnes Mercy Wahome na Josphat Nzuki.

Prof Japheth Micheni Ntiba ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa jumla ambapo atafanya kazi pamoja na wanachama wa kamati hiyo ikiwemo wenyekiti wa kamati ndogo nne na makatibu wao.

Kamati ya kuangazia mfumo wa ufadhili wa vyuo vikuu na taasisi za mafunzo ua ufundi stadi (TVETs) itahusisha  Prof. Karuti Kanyiga kama mwenyekiti akisaidiwa na Dibora Zainab Hirbo na wanachama wengine 30

Moses Njeru na Jemima Onsare ndio makatibu wa pamoja na ambao wataripoti kwa Diana Mutisya na Alex Kibet.

Walubengo Waningilo naye ataongoza kamati ya kushughulikia malalamiko yaliyoibuka kutokana na uainishaji wa wanafunzi katika vitengo vya kupokea ufadhili na mikopo ya serikali. Atasaidiwa na Lucy Machugu kama naibu mwenyekiti.

Kamati hiyo ina jumla ya wanachama 25. Margaret Campbell na Allan Chacha wanaongeza idadi hiyo wakiwa makatibu ambao watawasilisha matokeo yao kwa Darius Mogaka na Kingori Ndegwa.

Nayo kamati ya itakayohusika na muundo wa mikopo ya wanafunzi itasimamiwa na Robert Oduor Otieno akiwa mwenyekiti na Aaron Kiprotich Bett akiwa naibu mwenyekiti.

Tiberius Barasa na Clarise Osore ndio makatibu kwa sekritariati ya Geoffrey Monari na Emmanuel Abook katika  kamati hiyo yenye wanachama 18.

Kamati ya kuhakiki gharama za programu za vyuo vikuu itasimamiwa na Prof. Mohamed S. Rajab kwa usaidizi wa Patrick Malanga na jumla ya wanachama 31.