Mwanafunzi aliyeanguka katika bomba la maji taka aaga dunia

Mwanafunzi huyo aliaga duni akipokea matibabu katika hospitali moja kaunti ya Bungoma

Muhtasari

• Mwanafunzi wa shule ya upili ya Kamusinga aliaga dunia baada ya kuanguka katika bomba ya maji taka shuleni humo.

• Maafisa kutoka wizara ya elimu na wizara ya  usalama wa ndani wanachunguza kisa hicho.

Picha: HISANI

Bodi ya usimamizi wa shule ya upili ya Friends  School Kamusinga imetoa taarifa ya kifo cha mmoja wa wanafunzi wao aliyaeaga akipokea matibabu katika hospitali ya Lifecare alipopelekwa kwa matibabu baada ya kuanguka katika bomba la maji taka.

Katika taarifa iliyotiwa sahihi na mwenyekiti wa bodi ya usimamizi wa shule hiyo Prof. Moses Poipoi mnano tarehe 16 Septemba, barua hiyo inaarifu kuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo aliipa bodi hiyo taarifa kumhusu marehemu ambaye jina lake limebanwa.

Prof. Poipoi amekiri kuwa mwalimu mkuu alimfahamisha kisa ambapo mwanafunzi alianguka katika bomba la maji taka kisha kuokolewa na kupelekwa hospitali ya kaunti ndogo ya Kimilili kwa matibabu.

Marehemu alihamishiwa hospitali ya Lifecare kwa matibabu zaidi lakini baadaye aliaga.

Hata hivyo, wizara ya elimu inashirikiana na wizara ya mambo ya ndani katika uchunguzi kubaini kisa haswa cha matukio ya mwanafunzi huyo kuanguka katika bomba la maji taka.

Prof. Poipoi ameeleza kuwa kuna hali ya utulivu katika shule hiyo wakati bodi ya usimamizi ikiahidi kuzungumzia hatua za usalama katika shule hiyo.