Serikali imetangaza mageuzi ambayo inapania kufanya hili kuboresha usafiri wa ndege katika anga tua ya Jomo Kenyatta International Airport (JKIA).kutokana na taarifa ambayo ilitolewa na waziri wa fedha John Mbadi, akiwa na ushrikiano na katibu wa wazara ya uchukuzi na usafiri David Chirchir na waziri Rebecca Miano.
Katika taarifa hiyo waliosema kuwa serikali inapania kuboresha uwanja huo wa ndege hasa hali kwa huduma kwa wasafiri na kufikia viwango yva kimataifa.
Baadhi ya changamoto ambazo zinatafutiwa suluhu la kudumu ni pamoja na wasafari kuchukua mda mwingi wanaposubiri ndege na vile vile nafasi ya kuruhusiwa kuingia ndani na kuabiri ndege.
Aidha walisema kuwa watakabiliana na swala linalokabiliana na uwanja huo na kampuni ya Adani.Mbadi alisema kuwa wanapania kuimarisha itifaki ndiposa kuharakisha usafiri miongoni mwa wasafiri.
Aidha mawaziri hao walisema kuwa watafanya juhudi ndiposa kufanikisha usafiri kwani kwa sasa uwanja huo unafaa kuwa ukitumia njia za kielektroniki kusajili abiria wake na kupunguza shughli za kuwasilisha karatasi ambazo zimekuwa zikichangia pakubwa kupoteza mda na kuchelesha shughli za usafiri katika uwanja huo.
Aidha,serikali imesema itatoa mafunzo kwa wahudumu wa umma katika uwanja huo ndiposa kuweka viwango vya juu vya tajriba kwao na kutoa huduma bora kwa wasafiri.
Mageuzi haya yanajiri baada ya lalama kutoka kwa wasafiri ambao wamekuwa wakilalamikia foleni kubwa katika uwanja huo na kuchelewesha shughli zao za isafiri.
Aidha, wasafiri wengine walisema kuwa kumekuwepo na visa vya ulaji rushwa ndiposa ukubaliwe kuingia ama kuondoka vile vile kushughulikiwa kivyovyote vile.
Kufuatia kisa cha hivi karibuni ambacho mwanabiashara Diana Sherif alisema kuwa alitozwa kiwango kikubwa cha hela kufikisha mizigo yake Kenya.Bi Sherif alisema kuwa alicheleweshwa kwa takriban masaa matano huku akisema wahudumu walikuwa wakorofi na walikwamilia cheti chake cha usafiri pamoja na mizigo yake.