Gavana wa Kakamega Fernandes Baraza amemtaka waziri wa fedha John Mbadi kuwacha kuwapotosha Wakenya kwa kuwaambia kuwa tayari pesa za mgao kwa kaunti tayari zimetumwa kwenye akaunti za magatuzi.
Gavana huyo ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya fedha katika baraza la magavana amesema kuwa pesa ambazo kaunti zilipokea chini ya wiki moja iliyopita zilikuwa za mwezi Septemba ambazo serikali za kaunti zilikuwa zinadai.
Mnamo Jumatatu, waziri wa fedha John Mbadi alisema kuwa hazina ya kitaifa haidaiwi hela zozote na serikali za kaunti kwani shilingi bilioni 30.8 tayari zilitumwa kwa kaunti. Kwa mujibu wa Mbadi, kaunti sasa zinadai serikali kuu hela za mwezi Novemba.
Baraza la magavana limetishia kukatiza utoaji wa huduma kwenye kaunti ikiwa wizara ya fedha itakosa kuwapa hela wanazodai chini ya siku thelathini zijazo.
Kwa mujibu wa gavana Baraza, amesema kuwa pesa zikitoka kwa hazina ya kitaifa na kuelekezwa kwa kapu ya kaunti kwenye banki kuu ya Kenya huchukua chini ya wiki mbili kufika kwa akaunti za serikali za kaunti. Baraza amesema kuwa tangu pesa za mwezi wa Septemba kutolewa wiki jana, bado hazijaingia kwenye akaunti za kaunti.
Hata hivyo gavana huyo amesema kuewa kunahitajika mabadiliko
katika ofisi ya mtawala wa bajeti ili pesa zinapotokakatika serikali kuu
zinafikia kaunti ndani ya saa 48.
Aidha amesifia juhudi ambazo zimewekwa na wizara
ya fedha mwaka huu