logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Banki kuu ya Kenya yafanya marekebisho katika noti za shilingi ya Kenya

Noti mpya zitakuwa na sahihi ya gavana wa banki kuu na katibu mkuu wa hazina ya kitaifa

image
na Brandon Asiema

Yanayojiri20 November 2024 - 10:46

Muhtasari


  • licha ya mabadiliko yaliyofanywa kwenye moti hizo, vipengela vingine kwenye noti hizo zitasalia jinsi vilivyo jinsi noti zilivyotolewa mwaka wa 2019.
  • CBK imesema kuwa noti ambazo zinatumika zinabaki kuwa halali na zitaendelea kutumika licha ya noti zenye vipengele vipya kutolewa.

caption

Benki kuu ya Kenya CBK imetangaza mabadiliko katika sarafu ya Kenya kwa noti za shilingi 50, 100, 200, 500 na 1,000 kulingana na wajibu wake katika katiba ya Kenya kifungu cha 231(2) na kifungu cha 22(2) cha katiba ya Banki kuu ya Kenya. Awali mnamo Agosti 6, Banki kuu ya Kenya ilitangaza kufanya marekebisho katika muonekano wa sarafu ya Kenya.

CBK imesema kuwa licha ya mabadiliko yaliyofanywa kwenye moti hizo, vipengela vingine kwenye noti hizo zitasalia jinsi vilivyo jinsi noti zilivyotolewa mwaka wa 2019.

Vile vile, banki kuu ya Kenya imesema kuwa noti ambazo zinatumika zinabaki kuwa halali na zitaendelea kutumika licha ya noti zenye vipengele vipya kutolewa.

Mabadiliko yaliyofanywa kwenye noti hizo ni:

-          Noti zitakuwa na sahihi ya gavana wa benki kuu Dkt. Kamau Thugge.

-          Sahihi ya katibu mkuu wa hazina ya kitaifaDkt. Chris Kiptoo.

-          Mwaka wa kuchapishwa kwa noti hiyo, 2024.

-          Nyuzi mpya ya usalama yenye kubadilisha rangi ambayo ni tofauti kwa noti za kila kiwango.

Aidha banki kuu imesema kuwa noti hizo zenye vipengee vipya zitaanza kutolewa kwa noti za shilingi elfu moja, noti za viwango vingine vya shilingi mia tano, mia mbili, mia moja na hamsini zikitolewa katika michache ijayo.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved