Waziri wa ardhi Alice Wahome amesema kuwa mzozo kati ya jamii zinazoishi kwenye mpaka wa kaunti za Tharaka Nithi na Meru hauwezikutatuliwa kwa kuchora upya mpaka huyo.
Waziri Wahome aklizungumza mbele ya seneti, amesema kuwa watu wanaoishi upande wa Meru na ambao ni wa Jamii ya Tharaka Nithi wamekata kuwa hati miliki zao za mashamba haziwezi kubadilishwa kusoma Meru ilhali wao ni wa Tharaka. Jambo ambalo pia wakaazi wa jamii ya Tharaka wanaomiliki ardhi upande wa Meru wamekataa.
Waziri Wahome amefichua kuwa, mara ya mwisho alipozuru sehemu hiyo kupeana hati miliki za shamba, wazee wa Ncheke na viongozi wengine walimtaka asizungumzie maswala ya mipaka ya kiutawala.
Seneta wa Tharaka Nithi, Mwenda Gakaya Mo Fire alitaka kujua hatua ambazo serikali imepiga katika kubainisha mpaka baina ya Meru na Tharaka Nithi ili kutuliza mivutano baina ya jamii mbili zinazoishi sehemu hiyo.
Aidha, waziri Alice Wahome alijitenga na swala la kushughulikia mipaka ya kiutawala akisema kuwa bunge lazima lihusike kwa kutoa mwelekeo wa jinsi mpaka hiyo itabadilishwa.
Akitumia jukwaa hilo, waziri Wahome alielekeza ujumbe kwa magavana wa kaunti za Tharaka Nithi na Meru kuwa, mvutano kwenye mpaka huo hautamalizwa kwa kubadilisha mpaka. Wahome amesema kuwa ili kubadilisha mpaka, tume ya uchaguzi na mipaka IEBC ndio imetwikwa jukumu la kuratibu mipaka nchini na inaweza kufanya hivo baada ya bunge kuidhinisha.
Hata hivyo, waziri huyo amesema kuwa ana sehemu za uamuzi anaoweza kufanya kama waziri lakini wakaazi wa kaunti ya Tharaka Nithi kwenye eneo hilo la mpaka waliwafukuza maafisa kutoka wizara ya ardhi walipozuru mpakani hapo.
Kwa upande wa waziri Wahome, amesema kuwa hali ya mvurugano
itaendelea kushuhudiwa hadi pale wakaazi watakubali marekebisho katika hati za
umiliki wa shamba.