Kinara wa Narc-Kenya Martha Karua
Chama cha NARC Kenya kimepitisha maazimio mapya katika kongamano la kitaifa la wanachama wa chama hicho, kwenye mkutano uliofanyika jijini Nairobi ambapo wanachama wanapania kuleta mhemko mpya katika chama hicho.
Miongoni mwa maamuzi muhimu yaliyoafikiwa ni utekelezaji wa kutamatika kwa hatamu ya viongozi wa chama, huku mazungumzo yakiendelea ili kuweka kikomo katika hatamu ya uongozi wa chama kuwa mihula miwili Kiongozi wa chama hicho Martha Karua alisifu maazimio ya wanachama hao akisisitiza umuhimu wa kuipa chama hicho sura mpya na kufanya mpangilio kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2027
"Ninataka kushukuru wakuu katika chama kwa kuwapa wanachma wa NARC Kenya mamlaka ya kuunda upya chama tayari kwa 2027," Alisema Karua. Kama juhudi ya kubadilisha sura ya chama, wanachama hao waliafikiana kuibadilisha rangi yao rasmi ya chama kutoka rangi ya kijani kibichi na nyekundu hadi rangi ya zambarau na nyeupe, ila chama hicho kitahifadhi nembo yao ya ua la waridi na kauli mbiu ya chama hicho.
Wanachama hao vile vile waliafikiana w kuandikisha wanachama wapya kote nchini ili kujenga umarufu wa chama hadi mashinani kama njia moja ya kujiandaa kwa uchagzi wa 2027. Karua alishutumu serikali ya Ruto kwa kutoza wananchi ushuhuru wa juu zaidi.
"Tumekusanyika hapa ili kupambana na udhalimu wa kijamii unaolemewa na ushuru mkubwa unaotokana na utawala wa Ruto. Wakenya hawapati mahitaji ya kimsingi huku wanatozwa ushuru kupita kiasi na hata serikali kuvamia mifuko yao kupitia SHA/Shif.
" Haya yote yanajiri wakati uhusiano wa NARC kenya katika muungano wa Azimio ukizidi kudidimia, Wajumbe waliamua kuidhinisha kujiondoa kwa chama hicho kutoka kwa muungano huo wa Azimio, kufuatia barua rasmi ya Karua kwa Azimio kuashiria nia ya chama hicho kujiondoa.