Baraka ama laana?
Kaunti ya Kisumu nchini Kenya iliyo kwenye ukingo wa ziwa Victoria inakumbwa na mafuriko kila wakati wa msimu ya mvua kubwa. Mafuriko yanazidi kuwa janga kubwa zaidi ya kimazingira yanayotishia Kisumu na bonde la nyando, Mafuriko haya yana madhara makubwa kwa ustawi wa kijamii, kiuchumi ,kimazingira , kimwili na kisaikolojia.
Mvua kubwa iliyoshuhudiwa mwezi wa nne mapema mwakaa huu, iliwacha zaidi ya wakazi 14,000 bila makao na kuchangia uharibifu mkubwa huku ekari 1,756 za mashamba yenye mimea katika maeneo ya mabonde yakiharibiwa. Isitoshe masomo vile vile yalisambaratishwa kwani zaidi ya majengo ya madarasa ya wanafunzi wa chekechea vile vile yakiharibiwa huku wanafunzi wakibaki bila madarasa.
Uharibifu huo uliwaacha wakulima wengi wakihesabu hasara ya shilingi milioni 87.8. Baadhi ya mifugo 2,000 pia waliathiriwa na mafuriko kufuatia uharibifu wa malisho.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa ilipotaja kaunti ya Kisumu kama mojawapo ya maeneo ambayo yangepata idadi kubwa ya mvua msimu huu, wakaazi hao waliingiwa na wasiwasi kwani mpaka kufikia sasa hawajapata suluhu ya kudumu ya kujikinga dhidi ya mafuriko hayo licha ya hasara wanayopata katika msimu wa mvua kubwa.
Kufikia tarehe mbili mwezi wa Desemba mwaka huu. baada ya mvua kubwa kunyesha katika baadhi ya maeneo nchini. zaidi ya familia 700 zimekosa makazi katika kaunti ya Kisumu huku mafuriko yakikumba vijiji kadhaa vya Nyando na Nyakach.
Siku ya jumamosi serikali iliweza kutoa onyo dhidi ya uwezekano wa uharibifu kutokana na mvua kubwa inayoendelea nchini.
Katika eneo la Nyando, karibu wakaazi 400 kutoka maeneo ya Kakola, Kochogo, na Wawidhi walilazimika kutafuta hifadhi mbadala katika vituo mbalimbali vya uokoaji huku wengine wakilazimika kuishi na wandani wao walio maeneo salama.
Kutokana na naibu kamishna wa counti ndogo ya Nyando Richard Maranga maeneo hayo tatu ndio yameathirika zaidi.
‘’Mafuriko yametupata tena na tayari tunakabiliana na hali ngumu ya kimaisha . maeneo yetu yaliyoathirika zaidi ni pamoja na Kakola ambako karibu manyumba 200 zimesongwa na maji,’’ Alisema Maranga.
Katika eneo la Nyakach zaidi ya ekari 2,800 ya shamba iliweza kuharibiwa baada ya mto Miriu kuvunja kingo zake. Kutokana na tukio hilo chifu wa eneo la Nyakach ya juu alihakikisha kuwa wakaazi 300 waliweza kufurushwa kutokana na mafuriko hayo.
Kulingana na naibu wa chifu wa eneo la Nyakach Darwin Orina, juhudi za kutafuta usaidizi kutoka kwa mashirika za kiserikali inaendelea ili kusaidia wakaazi hao kujisaidia wakati wa janga hilo.
Mkaazi wa Sango, Maurice Owino alidai kuwa amepoteza mali yake yote baada ya mafuriko kuingia kwake.
‘’Boma yangu bado imezama katika mafuriko baada ya mto wa Miriu kuvunja kingo zake,’’ Alisema Maurice.
Katika hotuba iliotolewa Jumapili na wizara ya masuala ya ndani nchini ilisema kuwa iwapo mvua kubwa itaongezeka basi eneo la kaskazini mwa mashariki, kusini mwa mashariki, enoe la pwani, eneo la kati na kusini mwa bonde la ufa zitapata mafuriko kubwa Zaidi.
Katibu mkuu wa masuala ya kindani nchini Raymond Omollo alisema kuwa mafuriko hayo yanatarajiwa kupungua wiki ijayo. Aliongezea kuwa serikali imeanzisha mchakato wa kuhamisha watu walio kwenye mahali zilizoathirika.
‘’ Shuguli ya kuokoa watu inaendelea katika maeneo ya Kapuothe, Nanga, Lower Katuoro, Wigwa, na sehemu ya Dunga kaunti ndogo ya Kisumu ya kati ambako takriban boma 200 zimeathirika na Karibu ekari 100 ya mimea kusombwa na maji,’’ alisema Raymond Omollo.
Mafuriko haya yanakuja baada ya Rais Ruto kuahidi wakaazi wa Kisumu kujenga bwawa ambalo lina uwezo wa kubeba lita milioni 72 ya maji kwa matumizi ya nyumbani na kunyunyuzia mimea maji na hata kuzalisha nguvu ya umeme. Mradi huo ulitarajiwa kuwa baadhi ya suluhu ya kudumu ya mafuriko ya mto Nyando.