Katibu mkuu
wa wizara ya mambo ya ndani Dkt Raymond
Omollo ametoa mikakati ya kuimarisha usalama
nchini msimu huu wa likizo akiamuru maafisa wote waliokuwa katika likizo kurejea kazini mara moja.
Akizungumza na wanahabari katika jumba la Harambee jijini Nairobi, Raymond aliyekuwa ameambatana na wakuu wengine katika idara ya usalama ikiwemo inspekta jenerali wa polisi Douglas Kanja, alisema kuwa hatua hiyo ya kuwaamuru maafisa walio kwenye likizo kurejea kazini ni kutokana na haja ya dharura ya kikazi kwa matayarisho ya msimu wa shamra shamra za krismasi.
Katibu huyo mkuu aliongeza kuwa shughuli hiyo itajumuisha maafisa kutoka jeshi la ulinzi la Kenya, huduma ya kitaifa ya polisi, maafisa wa magereza, mafisa kutoka huduma ya wanyamapori ya Kenya na maafisa wa huduma ya misitu ya Kenya.
Wakenya sasa wanatarijia kuonana idadi kubwa ya maafisa wa usalama nchini kutokana na kuongezwa kwa vitengo maalum ikiwa ni pamoja na kitengo cha kikosi maalum ya kutumia silaha na mbinu za wanawake (SWAT), na maafisa wa siri, ambao wametumwa pamoja na maafisa kutoka kwa kitengo cha huduma ya jumla watasaidiana kudhibiti usalama nchini.ty
Omollo alihakikishia wakenya usalama wa sekta ya Utalii nchini akisema kuwa maafisa kutoka idara mbali mbali za kiusalama zitafanya kazi pamoja ili kuweka mikakati kabambe ya usalama kwa watalii wa humu nchini na wale kutoka nchi za kigeni katika mahoteli za pwani ya bahari na maeneo vivutio vya watalii nchini, hifadhi za taifa na mapori za wanyama.
‘’Tunawaomba wananchi kuwa waangalifu na kushirikiana na maafisa wa kisheria wakati wote wa msimu huu wa krisimasi ili kuhakikisha kuwa wakenya wote wako salama. Katika juhudi ya usalama ya kijamii, tunahimiza wananchi kuripoti visa vya uhalifu kwa kituo cha polisIkilicho karibu ama kupitia nambari za simu ya polisi ya 999, 112, 911 na #FichuakwaDCI0800722203,’’ Alisema Raymond.
Omollo aliongeza kusema kuwa huduma ya polisi ya kitaifa kwa kushirikiana na mamlaka ya kitaifa ya usalama wa uchukuzi (NTSA) itatekeleza utiifu wa sheria za trafiki kwa madereva wote wa kibinafsi na magari ya uchukuzi wa umaa.