logo

NOW ON AIR

Listen in Live

NCCK yatishia kuongoza maandamano ikiwa tume ya uchaguzi IEBC haitabuniwa chini ya wiki mbili

Muungano huo wa makanisa unaitaka mhakama na bunge la kitaifa kubuni tume mpya ya uchaguzi

image
na Brandon Asiema

Yanayojiri04 December 2024 - 08:12

Muhtasari


  • Kwenye mkutano, Askofu mkuu wa kanisa la Kiangilika nchini Jackson Ole Sapit aliitaka kanisa la St. Crispins ACK katika kaunti ya Bungoma kurejesha shilingi milioni tano zilizotolewa na rais kupitia gavana wa kaunti hiyo Kenneth Lusaka.
  • Viongozi hao wametoa notisi ya siku kumi na nne kwa mahakama kumaliza kesi zilizo mbele yake kuhusu kubuniwa kwa IEBC huku pia wakilitaka bunge la kitaifa kuharakisha mchakato wa kubuniwa kwa tume hiyo.


Muungano wa makanisa nchini NCCK umetishia kuongoza maandamano ya kitaifa kushinikiza mahakama na bunge la kitaifa kubuni tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ndani ya wiki mbili. Taarifa hiyo ya viongozi wa makanisa inajiri wakati utofauti unakithiri baina ya tabaka la wanasiasa na tabaka la waumini nchini na wananchi.

Katika mkutano wa NCCK uliofanywa katika mji wa Naivasha kwenye kaunti ya Nakuru, viongozi hao wametoa notisi ya siku kumi na nne kwa mahakama kumaliza kesi zilizo mbele yake kuhusu kubuniwa kwa IEBC huku pia wakilitaka bunge la kitaifa kuharakisha mchakato wa kubuniwa kwa tume hiyo.

Tangu kukamilika kwa muhula wa tume ya uchaguzi na uratibu wa mipaka IEBC mnamo Januari mwaka 2023, tume mpya ya IEBC yenye jukumu la kuendesha uchaguzi mkuu nchini ingali kubuniwa licha ya baadhi ya maeneo bunge na wadi nchini zikikosa uwakilishi kutokana na kufariki kwa viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi wa 2022 na katika sehemu nyingine, mahakama ikifutilia mbali ushindi wa viongozi waliokuwa wametangazwa na IEBC.



Kwa sasa ni takribani  miaka miwili tangu muhula wa makamishma ya IEBC waliokuwa chini ya mwenyekiti Wafula Chebukati kukamilika na makamishna wapya wangali kuteuliwa.

Kwenye mkutano huo pia, Askofu mkuu wa kanisa la Kiangilika nchini Jackson Ole Sapit aliitaka kanisa la St. Crispins ACK katika kaunti ya Bungoma kurejesha shilingi milioni tano zilizotolewa na rais kupitia gavana wa kaunti hiyo Kenneth Lusaka. Kwa mujibu wa Ole Sapit, kanisa hilo kupokea shilingi hizo kutokakwa wanasiasa alizotaja kuwa pesa za ufisadi ni dharau kwa makanisa mengine kama vile kanisa Katoliki ambalo kupitia Askofu wake wa Dayosisi ya Nairobi Philip Anyolo alikana michango ya helaya wanasiasa kubabidhiwa mapadri.



Makanisa nchini yamekuwa mstari wa mbele kuwajibisha serikali yakitaka wanasiasa kutimiza ahadi walizotoa kwa wananchi wakati wa kampeni pamoja na kurahisisha hali ya uchumi kwa wananchi.

Mkutano wa NCCK unajiri wiki chache baada ya baraza la Maaskofu wa Kikatoliki nchini kuilaumu serikali kwa kukosa kuwasikiza Wakenya wakati wa kutekeleza miradi inayohusu wananchi. Baraza hilo la Maaskofu wa kanisa Katoliki, liliishtumu serikali ya rais William Ruto kwa kuasisi mamlaka ya bima ya afya SHA na mtaala mpya wa elimu wa CBC kwa kukosa kuhusisha wananchi vikamilifu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved