Ofisi ya mkurugenzi wa mshataka ya umma ODPP imejivunia mafaniko iliyoafikiwa chini ya mwaka mmoja tangu mkurugenzi wake Renson Ingonga kuchukua uongozi wa DPP mnamo Januari 20, mwaka wa 2023.
Katika hafla ya kuzindua mpangilio wa mikakati ya ODPP ya kuanzia mwaka 2023 hadi 2027 mnamo Jumatano katika taasisi ya mafunzo ya uendeshaji wa mashtaka jijini Nairobi, idara hiyo imeweka wazi hatua muhimu ambazo ODPP imefanikisha tangu kuingia kwa Renson Ingonga.
Kwenye baadhi ya mafanikio yake kati ya kesi ambazo ODPP ilifaulu kushinda ni ikiwemo kesi ya ufujaji wa shilingi milioni 2 katika eneo bunge la Embakasi Kusini ambapo meneja wa zamani wa mfuko wa maendeleo ya eneo bunge CDF Peter Mukhanji pamoja na mkewe walipatikana na hatia.
Kwenye kesi hiyo, mahakama mnamo Mei 27, 2024 iliamuru Mukhanji na mkewe kulipa faini ya shilingi milioni 3 au kuhudumu kifungo cha miaka 3 kwa ufisadi uliohusu usambazaji wa kompyuta katika eneo bunge hilo.
Vile vile, Renson Ingonga alichaguliwa rais wa chama cha wandesha mashtaka barani Afrika katika hafla iliyoandaliwa nchini Morocco mnamo Julai 11, 2024. Mafanikio haya, kwa mujibu wa ODPP, inaashiria jukumu la Kenyakatika kuimarisha viwango vyake vya haki na kisheria barani Afrika.
Pia, ODPP kwenye hatua ilizoafikia ndani ya mwaka mmoja,
imesema kwamba ilifanikisha kufikishwa mahakamani kwa mchungaji matata Paul
Mackenzie ambaye alihusishwa na vifo vya mamia ya waumini wake katika shamba la
Shakahola. Mackenzi alishtakiwa kwa hatia ya ugaidi huku pia akikabiliwa na
shtaka la mauaji ya halaiki ya watu.
Chini ya mwaka mmoja wa Ingonga, ODPP pia
ilizindua chumba cha kuhoji waathiriwa wa madhila mabli mbali ambao ni watoto.
Chumba hicho kinasaidia katika kurekodi ushahidi kutoka kwa watoto kabla ya
kuwasilishwa kortini ODPP ikisema kwamba chumba hicho kimesaidia kutokomeza
uonevu pamoja na kuwepo kwa mazingira salama ya mashahidi kutoa maelezo yao
bila uoga.