Mamlaka ya ukusanyaji kodi nchini KRA imetangaza kuimarika kwa mapato iliyokusanya ndani ya kiezi mitano ya kwanza katika mwaka wa kifedha wa 2024/2025.
Kwa mujibu wa mamlaka hiyo kwenye ukurasa wa X, imesema kwamba mapato yaliyokusanywa yalipita shilingi triolini moja kufikia tarehe 30 mwezi Novemba mwaka wa 2024 ikilinganishwa na mapato ya mwaka uliopita wa kifedha katika muda sawia.
KRA imesema kwamba mwaka wa kifedha uliopita, jumla ya shilingi bilioni 963.746 zilikusanywa katika kipindi sawia, huku mwaka wa kifedha wa 2024/2024, jumla ya shilingi trilioni 1.005 zilikusanya kati ya mwezi Julai na Novemba.
Aidha katika taarifa hiyo ya KRA, ongezeko hilo la mapato limeashiria asilimia 4.3.
Mamlaka ya KRA, inalenga kukusanya takribani shilingi trilioni 2.704 kufikia mwisho wa mwaka wa kifedha 2024/2025 ikielezea matumaini ya kuafikia malengo haya.
“Ikiwa na mwelekeo wa juu zaidi, mamlakaina uhakika wa kufikia lengo hili na kudumisha uchumi wa Kenya.” Iliandika KRA kwenye ukurasa wake wa X.
Vile vile, kwenye taarifa hiyo, kodi za ndani kati ya mwezi
Julai na Novemba ziliimarika kwa asilimia 3.5 kutoka shilingi bilioni 621,984
mwaka jana na kufikia shilingi bilioni 643,790 mwaka huu.